Mwigizaji Nora Amchana Live Kajala Masanja

Nyasamaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
1,055
Reaction score
595




MWIGIZAJI kiwango enzi hizo Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora' aliyepotea kwa muda, ameibukia kwenye Runinga ya EATV na kumbutua staa wa mwenzake, Kajala Masanja kwamba, anatumia nafasi ya kuonekana kwenye filamu kujipatia wanaume kama si mabwana!

Akizungumza kupitia Kipindi cha Mkasi kinachoratibiwa na Mtangazaji Salama Jabir, Jumatatu iliyopita, Nora alisema fani ya uigizaji imevamiwa kwa sasa kwani kuna watu ambao wanaingia kwenye gemu ili wauze sura na kuonekana na wanaume wapate ‘soko' kiulaini.

Aliongeza kuwa, watu hao kupitia vitendo hivyo wamekuwa wakiichafua tasnia kiasi cha wote kuonekana hawafai (samaki mmoja akioza, ni wote).

Nora alikwenda mbali zaidi alipoulizwa na Salama ni nani na nani hawafai na nani wanafaa, alishindwa kuwataja kwa majina moja kwa moja lakini mtangazaji huyo akaomba ataje majina yeye kisha Nora aseme kama anafaa au hafai!
Salama: "Kajala."

Nora: "Huyo hamna kitu."
Salama: "Batuli."
Nora: "Huyo pia hamna kitu."
Salama: "Lulu."
Nora: "Huyo safi."

Salama: "Mlela (Yusuf)."
Nora: "Huyo hamna kitu."
Salama: "Steve Nyerere."
Nora: "Huyo hamna kitu."

Salama: "Hemed (Suleiman)."
Nora: "Hamna kitu hapo."
Juzi gazeti hili lilimsaka Kajala kwa njia ya simu hakupatikana, lakini mmoja wa watu wake wa karibu alisema staa huyo ameshangaa sana Nora kutaka kurudi juu kwa kutumia jina lake.

"Kajala amezima simu, lakini kamshangaa sana Nora, alishazimika, sasa anaonekana anataka kuwaka tena kwa kutumia jina lake," alisema mpambe huyo.
GPL
 
haya magazeti sijui yanapata faida gani watu waligombana
 
Awa jamaa waongo sana... Nilitazama iyo show na jibu la Hemed halikuwa hilo,alisema anafaa. Shigongo utachomwa moto mbaya sana kwa kulisha wajinga uongo na kuchonganisha.
 
Awa jamaa waongo sana... Nilitazama iyo show na jibu la Hemed halikuwa hilo,alisema anafaa. Shigongo utachomwa moto mbaya sana kwa kulisha wajinga uongo na kuchonganisha.

Dah,mkuu hiyo avatar yako huwa inaniogopesha sana...siku ukiibadili nitafurahi mno,leo nimejikaza kuku quote....
 
Binafsi naona Nora anatapa tapa ili apate keek ya kurudi kwenye game,Akubali kashapokeza kijiti zama zake zimepita na sio kuhangaika na kulazimisha kusikika masikioni mwa watu.

Mambo yake yanamwendea kombo kila anachofanya chenga,juzi juzi katoka kukimbiwa na mume,sura imechoka haiuziki kwenye tasnia hivyo bora atafte namna nyingine ya kutoka kimaisha na sio kuponda watu ambao wanamzidi kila kitu.
 
Alisema hemed,kajala wanafaa
Acheni kuchonganisha watu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mleta mada kama na yeye kaedit na kuongeza ukuda wake.Hata mimi niliangalia Mkasi monday huu jamaa kaweka yake.Nora hakusema Hemed hamna kitu nakumbuka chaaah.
 

Wanamzid kwa lip labdaa hebu fafanua??? Maon aliyotoa yanaingiliana vp na maisha yake binafsi???? Makubwa haya
 
Awa jamaa waongo sana... Nilitazama iyo show na jibu la Hemed halikuwa hilo,alisema anafaa. Shigongo utachomwa moto mbaya sana kwa kulisha wajinga uongo na kuchonganisha.

Hili jitu la hovyo sana pamoja na crue yake yote hopless
 
hivi Global mkitokea siku mkaandika habari za ukweli mtakufa? acheni kuongea chumvi ili lizuke bifu mpate cha kuandika. Nina wasiwasi na taaluma yenu acheni kupotosha umma
 
NG'WIZUKULU SHILALA,si alimuona kwenye TV?nayeye walewale
 
Wanamzid kwa lip labdaa hebu fafanua??? Maon aliyotoa yanaingiliana vp na maisha yake binafsi???? Makubwa haya

Sijaingilia maisha yake,binafsi ninachozungumzia ni tasnia ya filamu.Ukweli kwamba kashapokeza kijiti na kupotea machoni mwa watazamaji na wapenzi wa filamu za kibongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…