Mwigulu: Acheni ubingwa wa kuorodhesha matatizo

Mwigulu: Acheni ubingwa wa kuorodhesha matatizo

Kama kuna matatizo katika Utawala wa Nchi yetu tukiyarodhesha tukamjuza Maza kuna ubaya katika hilo?

Tuliorodhesha tatozo la Tozo kuwa lunatubana sana ukasema "hamieni Burundi" ni bora ungetuambia hizo fedha walizotoa Wajerumani zitafanyiwa nini mbona uko kimya sana kwenye hilo.
 
Kwenye scientific procedures to solve the problems kinachotakiwa hatua ya kwanza ni Identification of the problem

Sasa utatambuaje tatizo bila kuorodhesha?

Waache watu waorodheshe matatizo swala la kutatua ni mchakato na wao wanaweza kuondoka madarakani wangali hawajatatua matatizo
 
Mbona yeye aliorodhesha kwanza aina ya Tozo kisha akaanza kututoza. Tatizo liko wapi hapo Wanabchi kuorodhesha Matatizo?
 
Ili tuweze kutatua matatizo yetu hatuna budi kuyaorodhesha kwanza, tunahitaji mabingwa wa kuorodesha matatizo kama hatua ya awali kuelekea kwenye kupata ufumbuzi wa matatizo....hata PhD yake aianza kuandika Problem Statement kablaa ya kufika kwenyee chapter ya Results....huyu anakuwa kama sio msomi bana😆🤸🐒
 
No problem, tatizo langu namba moja ni uwepo wake kama waziri wa fedha, sioni cha maana anachofanya zaidi ya kubuni tozo za kila aina na kuzidi kumkandamiza mtanzania kiuchumi, na pia, maprofesa wa uchumi wameshasema tozo hazikuzi uchumi wa taifa.

Solution yangu, Mwigulu anatakiwa kuondolewa kwenye wizara ya fedha, ameshaonesha sio creative wa kubuni vyanzo vya mapato kwa serikali bila kumuumiza mtanzania.
 
Screenshot_20221125-170130.jpg
 
Kwani mtu akiorodhesha ambalo limeshafanyiwa kazi si kumuambia tu hili tumelifanyia kazi na limetatuliwa hivi abc. Hiyo si ndio kazi ya Kiongozi na Uongozi?

Tusaidieni la ughali wa maisha mmeliona na kulitatua vipi? Kwa nini kuingia kwa mfano bidhaa ya sukari ya Bagamoyo sugar sokoni hatuoni impact yake kwenye kushuka kwa bei ya sukari sokoni?
 
Back
Top Bottom