Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
“Kodi ya pango itakusanywa na TRA” Mwigulu"
Waziri wa fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba amesimama Bungeni leo September 20, 2022 na kutoa kauli ya Serikali kuhusu tozo ambapo ameeleza marekebisho yatakayofanyika a kuanza kutumika kuanzia October 1, 2022.
Waziri Mwigulu amesema “Serikali inafuta utaratibu wa kodi ya zuio inavotokana na pango kukusanywa na
Mpangaji na badala yake jukumu hilo linarejeshwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa utaratibu utakao bainishwa kwenye kanuni”.
“Napenda kusisitiza kuwa kodi ya zuio ya pango sio ya Mpangaji bali inapaswa kulipwa na Mpangishaji ambaye ndiye anapokea mapato kutokana na uwekezaji au biashara ya kupangisha”
“Utaratibu huo umekuwa ukitumika kwa muda mrefu kwenye nyumba za biashara na nyumba zinazopangishwa kwenye makampuni au mashirika yanayofunga ritani za kodi