Mwigulu kuongoza waombolezaji kumuaga ofisa wa TRA, Aman Simbayao aliyeuawa kwa kushambuliwa

Mwigulu kuongoza waombolezaji kumuaga ofisa wa TRA, Aman Simbayao aliyeuawa kwa kushambuliwa

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwili wa aliyekuwa mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Aman Simbayao aliyefariki dunia kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira eneo la Tegeta kwa Ndevu, jijini Dar es Salaam, utaagwa leo Jumapili, Desemba 8, 2024.
IMG_1362.jpeg

Shughuli ya kuaga mwili huo itafanyika viwanja vya michezo vya TRA Kurasini kuanzia saa 6 mchana na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba anatarajia kuwaongoza waombolezaji kuaga mwili huo.

Pia, Soma: Jeshi la Polisi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za mauji ya Mtumishi wa TRA Amani Simbayao kutoka tukio la Tegeta

Simbayao ni miongoni mwa maofisa watatu walioshambuliwa na wananchi eneo la Tegeta kwa Ndevu, usiku wa Desemba 5, 2024 ambao walizuia gari aina ya BMW x6 lililodaiwa kutokuwa ndani ya mfumo wa mamlaka hiyo.

Watumishi hao wa TRA walipojaribu kulizuia gari hilo, kuliibuka mzozo hadi dereva akapiga kelele kuomba msaada akidai anatekwa, jambo lililosababisha wananchi kuwashambulia kwa mawe maofisa hao.
 
Back
Top Bottom