Dkt. Mwigulu Nchemba amesikika hadharani akisema miamala ya simu haijaathirika na uwepo wa tozo mpya kwa jina la uzalendo:
Hii si kweli na huu ni ushahidi ukiwahusisha mawakala na wenye mitandao:
Achilia mbali kuwa wengi wetu tuliokuwa wateja wa shughuli hizi za miamala tumeachana nazo.
Ikizingatiwa kuwa siku za nyuma aliwahi kututaka tuhamie Burundi kama haturidhii tozo hizi, ni wazi kuwa bwana Mwigulu amepoteza uhalisia na maisha yetu:
1. Tulipo sisi tunakabiliwa na janga la Corona.
2. Kutokana na #1, hata matibabu ya gonjwa hili linapotukumba tunajigharimia wenyewe.
3. Kutokana na #1, mapato yetu kwenye biashara zote zikiwamo za usafirishaji, utalii, mipakani, cross border, nk zimedorora kama si kufa kabisa.
4. Kodi za mafuta ya magari zimepanda na kutuongezea gharama zaidi za maisha katika nyanja zote.
5. Tunawasikia wenzetu wakipeana takrima za magari na majumba ya mabilioni kwa pesa zetu.
6. Wamejilimbikizia malipo lukuki yasiyolingana na tija wala uzalishaji wao, sisi tukiwagharimia.
7. Hakuna hatua zozote tuzionazo zikichukuliwa kuhusiana na wizi au ubadhirifu kwa mujibu wa ripoti za CAG.
8. Hakuna hatua zozote tunazoziona zikichukuliwa kuhusiana na mashirika sugu yanayotuzalishia hasara kila wakati.
9. Nk
Serikali inaonekana janga la Corona wao wala haliwahusu hata kidogo. Wao wanaendelea na mipango yao kama vile kila kitu ni shwari.
Nia yao inaonekana ni kutukamua sisi tu na bila huruma hata kama tuko hoi vitandani tukichungulia makaburini.
Serikali ya namna gani isiyokuwa na kuwajibika kwa watu wake hata kwenye majanga kama hivi?
"Mheshimiwa Waziri kwanini asijiuzulu tu kwenye mazingira haya?"