Bubu Msemaovyo
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 4,120
- 3,468
Hivi karibuni tumesikia kwamba Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Mwigulu Nchemba anadaiwa kuwapeleka vijana katika makambi ya Itende na kwingineko ili wapate mafunzo kwa kazi maalumu ya kichama. Kufanya hivyo ni uvunjaji wa Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania. Mwenye mamlaka hayo ni Serikali pekee.
SURA YA TISA
MAJESHI YA ULINZI
147.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote. (2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano yaweza, kwa mujibu wa sheria, kuunda na kuweka Tanzania majeshi ya aina mbalimbali kwa ajili ya ulinzi na usalama wa nchi na wananchi wa Tanzania. (3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.
Hivi vikundi vyenu ni batili futeni mnatuandalia majambazi tu!!