LESIRIAMU
JF-Expert Member
- Feb 12, 2008
- 9,006
- 14,536
Katika hali ya kushangaza, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba amewaamuru madiwani wa Jimbo la Iramba ambao amewaweka yeye madarakani wasitishe uamuzi wa kujenga shule eneo la Ruruma kata ya kiomboi ambalo watoto wanatembea hadi kilomita 15 mpaka 20 kuzifuata shule za sekondari zilipo kwa sasa. Badala yake ameamuru shule ya pili sasa ijengwe karibu na shule nyingine eneo la Kizega kama kilomita 3 tu toka ilipo shule nyingine ya New Kiomboi sekondari.
Sababu kuu ya Waziri ni kwamba eneo la Ruruma lilimkaribisha Tundu Lisu kiongozi wa Uponzani kulala kijijini hapo baada ya Mwigulu Nchemba kuamuru asipewe chumba guest house yeyote hapo mjini kiomboi na kuzilipa guest houses hizo zote ili Tundu Lisu asilale Kiomboi alipofanya Ziara huko.
Sasa viongozi wa namna hii ni hatari kwa jamii yetu. Hh. Rais Dk. Samia Suluhu Hasan aingilie kati ili shule Ijengwe Ruruma na kupunguza mateso kwa watoto wetu na fedha anazotoa ziwasaidie wananchi vizuri na kwa usawa na kwa haki katika huduma.
Na ikimpendeza Mh. Rais amuwajibishe Mwigulu Nchemba kama wengine anavyo wawajibisha ili kuliokoa Taifa na viongozi wa hovyo wa aina hii.