Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Mtanisamehe!
Kwakuwa sisi watanzania ni watu tusioweza kuungana kupinga jambo linaloumiza wachache, naomba makali yo tozo yaendelee na zaidi kodi ya kichwa ianze kukusanywa kwa vitendo.
Wapinzani waliteswa na kunyanyswa sana lakini kuna wenzetu walikuwa wanabeza Kwakuwa hayawahusu na wakiamini wao wako salama.
Kundi lingine la watu waliokandamizwa ni la wanufaika wa Bodi ya Mikop ambao waliongezewa makato almost mara mbili na walipolalamika, kuna watu waliwabeza kwa maneno kama lipeni na wengine wasome, n.k.
Wengine ni watumishi wa umma ambao walikaa karibu miaka sita bila kuongezewa mishahara, na walipolalamika, kuna watanzania waliwaambia kama mshahara haitoshi waache kazi na kejeli nyingine nyingi.
Tukasikia habari za watu kupunguziwa mishahara tukafurahia utadhani hiyo mishahara mikubwa haikuwa na baraka za serikali.
Mifano iko mingi tu. Sasa leo limekuja hili la tozo linalotugusa wote, karibu kila mtu analalamika na wala hakuna anaehamia Burundi kama tulivyoambiwa.
Ukweli ni kwamba, watanzania hatuwezi kuungana kwa nguvu kupinga mambo ya aina hii kwasababu wengi wetu tumejaa ubinafsi (sijaguswa kwanini nihangaike?). Matoke yake ndio haya yanayoendelea leo hii.
Labda niulize, walipoongeza makato ya Bodi ya Mikopo karibu mara mbili, watanzania tuungeungauna kupinga makato yale, leo wangetuletea hizo tozo na kutambia tuhamie Burundi kama hatuzitaki?
Mimi nasema kodi ya kichwa irudi na utekelezaji wake uanze mara moja pengine ipo siku tutaungana kama watu wa mataifa mengine wanavyofanya pale watawala wanapojisahau au kutotimiza wajibu wao.
Mtoto umeleavyo, ndivyo akuavyo-Waswahili.