Mwijaku alishindwa nini kununua kiwanja kinachoendana na mipango yake ya ujenzi? Kampuni ya ujenzi ilishindwa kumshauri?

Mkuu bado unaamini ile nyumba ya Mwijaku ni 1.3 B?

Ile nyumba hata 200 milioni haifiki..
Usibabaishwe na marangi pamoja na swimming pool juu ya paa.
 
Nyie wanawake mna kazi sana. Wivu husuda na kijicho. Halafu unaandika kama sisi wote tunamfahamu huyo mwidaku. Hapo utakuta mmechukuliana mabwana sasa ndo manaanza leta habari hizo JF
 
Kwani higo 1.2b unadhani alikuwa nayo bank au ni hesabu baada ya kumaliza ujenzi
Alikuwa anadunduliza na kuitupa kwenye ujenzi. Hata msukuma mkojoteni anaweza kujenga nyumba ya milioni 30 kwa kudunduliza halafu mtanzania ataanza kumkosoa kwamba aah hiyo hela ungefungua hardware. Hivi wanafahamu maana ya kudunduliza hawa watu??
 
Webongo wengi ukiwashauri utasikia we unayo, mchawi, wivu nk. Hawawezi kupokea ushauri au challenge kama watu wazima. Bado wabongo wengi wana akili za kitoto. Namaanisha wabongo wengi wamekomaa miili ila akili zao wengi za kitoto.
 
Mkuu bado unaamini ile nyumba ya Mwijaku ni 1.3 B?

Ile nyumba hata 200 milioni haifiki..
Usibabaishwe na marangi pamoja na swimming pool juu ya paa.
Mkuu Ila na wewe umeshusha sana, haifiki 200M???. Hivi gharama ya nyumba huwa hihusishi na thamani ya kiwanja?

Mtu akisema katumika bil.1 siyo kwamba anajumlisha gharama ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa kiwanja?
 
Mnapojadili hii mada wekeni kwenye mbongo then maneno Great thinkers ; jukwaa limeandaliwa kwa ajili ya kujadili hoja siyo kusifu na kupeana moyo.

Kama huna uwezo wakufahamu nafasi ya bilioni moja kwenye ujenzi usijitutumue kujadili kwa sababu tu unataka kusema; katika ujenzi Ile nyumba ya Mwijaku haina thamani ya bilioni moja na milioni mia tatu.

Lakini kwa upande wa pili hoja hapa siyo thamani ya nyumba, ni kiwanja na eneo alipojenga. Tukubali kwamba huyu kakosea kujenga, alipaswa kujenga nyumba kwenye eneo ambalo limepimwa na lina nafasi ya kupata oxygen.

Lakini pia ifahamike hapa hatupo kumshauri Mwijaku, tupo kuwashauri wengine wanaotamani kujenga.....tunawafumbua macho.

Jambo jingine ambalo wasanii wanapaswa kulizingatia kwa huko tuendako ni utajiri unaoendana na uwezo wa kulipa kodi. Mwijaku angetamka 1.3 bilioni kwenye nchi zilizoendelea hoja ingekuwa anapata wapi hizi fedha? Analipa kodi kutokana na faida ya mapato yake? Kibongo bongo hakuna mtu anayejali analysis ya kodi za nchi na ndiyo maana hatuna tatizo na kutaja figure kubwa.

Kwa wale tunaopanga kujenga lazima tujione kwenye nafasi hiyo. Wapo wanasiasa wengi na watumishi wa umma wamekimbia majumba yao na makazi yao baada ya kuteuliwa kwa sababu walishindwa kujipanga wajenge wapi kabla yakupewa madaraka.

Tununue maviwanja siyo viwanja
 
Kama amejenga ni jambo jema sana wacha life liendelee maana hata asingejenga still angeendelea kulala ndani na si nje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…