Mwijaku aongeze umakini anapokuwa ughaibuni

Mwijaku aongeze umakini anapokuwa ughaibuni

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Siyo mpenzi sana wa kufuatilia wala kuongelea maisha binafsi ya mtu ila hili naomba nitoe kama angalizo kwa muhusika tajwa ila inaweza kufaidisha na wengine.

Mwijaku amekuwa na tabia ya kupost video akiwa huko ughaibuni. Nakumbuka video zake kule Ivory Coast kwenye AFCON kama kumbukumbu zangu zipo sahihi. Kama sikosei niliwahi ona video yake nyingine kule Uarabuni kama sikosei na kuna hii nimeiona jana au juzi akiwa huko Marekani.

Katika video hizi zote, Mwijaku anaonekana akitembea kwa miguu barabarani katika hali inayohatarisha maisha yake na watumiaji wengine wa barabara. Wenzetu wana sheria za "jaywalking" ambayo inahusiana na kutembea au kuvuka barabara bila kufuata sheria. Ile video ya Mwijaku akiwa Marekani ni "jaywalking" moja kwa moja na watu huwa wanakamatwa na kushtakiwa kwa kosa hilo.

Sehemu kama Marekani ambapo kupata viza ni kimbembe, anaweza kutokea hater mmoja akaforward video zake kwa wakulungwa akapigwa pini asikanyage tena huko.

Holaaa.

PS. Sina ukaribu naye ila ningekuwa nao ningemtumia huu ujumbe katika mawasiliano yake binafsi.
 
Siwezi kusima wala kufuatilia habari yoyote ya mtu kama huyu!!!??? Yan nikiona tu picha yake au habari zake na skip!!! He is silly!!!! Plus idiot
 
Hii jamaa ni kima kabisa kasoro mkia tu.
Huenda na mkia anao.
Ningekuwa rais wa nchi hii nahisi ningekuwa Dikteta.
Mtu kama huyu ana aibisha nchi yaani akitua airport ni moja kwa moja Segerea🤣🤣🤣
 
Anashobokea kuwasalimia wazungu wanamkataa..naona ni aibu sana kwa kweli..kiingereza chenyewe sasa anachoongea ni aibu zaidi.
 
Back
Top Bottom