Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mtoto wa Tandale, Diamond Platnumz, Mswahili aliyepitia changamoto nyingi kwenye safari yake ya muziki, lakini akatoboa na kuwa nyota mkubwa wa Bongo Flava. Tangu enzi za wimbo wa "Kamwambie" mwaka 2010, uliompa umaarufu mkubwa na kufungua milango ya mafanikio yasiyopimika.
Ndoto zake hazijaishia kwenye muziki pekee, bali zimefika pia kwenye biashara, ambapo wakati akizindua rasmi tamasha la #WasafiFestival2024 alitangaza kuwa ana ndoto ya kuwa tajiri namba moja Duniani, yaani kuvaa viatu vya Elon Musk, CEO wa Tesla Motors mwenye utajiri wakutupwa na binadamu tajiri zaidi duniania.
Kauli iliyowashangaza wengi na kuzua mijadala mpaka kwa mashemeji zetu Kenya.
Mpenja alisema "Usimkati mtu tamaa!" akisherehesha goli la Kibu D, mechi ya Watani wa Jadi (Simba na Yanga), wakati Wananchi Wakiimbiswa Rege pale Lupaso. So hata Simba la Masimba anaweza kwani kitambo tu amekuwa akitumia jina la Chibu Dangote, jina la Bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote mwenye utajiri wa Dola bilioni 11.9, kama inspiration ya kuelekea ndoto yake ya utajiri.
Si unajua lifestyle ya DC wa Insta, Mwijaku, wala hakupoa jambo bado lamoto! Akaibuka na kupinga kauli ya Diamond akisema kuwa hajafikia hata 40% za utajiri wa mfanyabiashara Fred Vunjabei, hivyo bado anasafari ndefu.
Ooooh! hitmaker huyo wa Komasava si amejibu kwa kusema uandaliwe mdahalo kati yao na kila mmoja aoneshe mali zake, ili iwe funzo kwa wengine.
Unadhani, Fred Vunjabei ataikubali challenge hiyo?
Soma ==> Ni Diamond Platnumz ukipenda mwite Warren Buffett wa Bongo
Unadhani, Fred Vunjabei ataikubali challenge hiyo?
Soma ==> Ni Diamond Platnumz ukipenda mwite Warren Buffett wa Bongo