Mtoto wa Tandale, Diamond Platnumz, Mswahili aliyepitia changamoto nyingi kwenye safari yake ya muziki, lakini akatoboa na kuwa nyota mkubwa wa Bongo Flava. Tangu enzi za wimbo wa "Kamwambie" mwaka 2010, uliompa umaarufu mkubwa na kufungua milango ya mafanikio yasiyopimika.
Ndoto zake hazijaishia kwenye muziki pekee, bali zimefika pia kwenye biashara, ambapo wakati akizindua rasmi tamasha la #WasafiFestival2024 alitangaza kuwa ana ndoto ya kuwa tajiri namba moja Duniani, yaani kuvaa viatu vya Elon Musk, CEO wa Tesla Motors mwenye utajiri wakutupwa na binadamu tajiri zaidi duniania.
Kauli iliyowashangaza wengi na kuzua mijadala mpaka kwa mashemeji zetu Kenya.
Mpenja alisema "Usimkati mtu tamaa!" akisherehesha goli la Kibu D, mechi ya Watani wa Jadi (Simba na Yanga), wakati Wananchi Wakiimbiswa Rege pale Lupaso. So hata Simba la Masimba anaweza kwani kitambo tu amekuwa akitumia jina la Chibu Dangote, jina la Bilionea wa Nigeria, Aliko Dangote mwenye utajiri wa Dola bilioni 11.9, kama inspiration ya kuelekea ndoto yake ya utajiri.
Your browser is not able to display this video.
Si unajua lifestyle ya DC wa Insta, Mwijaku, wala hakupoa jambo bado lamoto! Akaibuka na kupinga kauli ya Diamond akisema kuwa hajafikia hata 40% za utajiri wa mfanyabiashara Fred Vunjabei, hivyo bado anasafari ndefu.
Ooooh! hitmaker huyo wa Komasava si amejibu kwa kusema uandaliwe mdahalo kati yao na kila mmoja aoneshe mali zake, ili iwe funzo kwa wengine.
Unadhani, Fred Vunjabei ataikubali challenge hiyo?
Mambo mengine sio ya kushabikia sana sababu ukweli unajulikana.
Diamond ni Hustle zake na watu wakubwa kumsapot hadi pale alipofikia.
Vunja Bei nae ni kimvuli cha wachina kuleta bidhaa bongo.
Sio inshu Tajiri kukuachia uandike Mali yako Kwa Jina lako..Sababu wapo wengi wanafanya hivyo sababu matajiri wanajua huna pakukimbilia yaani huwezi kuwakimbia MaBig Fish labda uwe maiti.
Mambo mengine sio ya kushabikia sana sababu ukweli unajulikana.
Diamond ni Hustle zake na watu wakubwa kumsapot hadi pale alipofikia.
Vunja Bei nae ni kimvuli cha wachina kuleta bidhaa bongo.
Sio inshu Tajiri kukuachia uandike Mali yako Kwa Jina lako..Sababu wapo wengi wanafanya hivyo sababu matajiri wanajua huna pakukimbilia yaani huwezi kuwakimbia MaBig Fish labda uwe maiti.
Baada ya Mwijaku kumuhusisha Mfanyabiashara Fred Vunja Bei, kwenye kauli ya Diamond kuhusu utajiri ambapo alisema mwanamuziki huyo hafikii hata asilimia 40% ya utajiri wa Vunja Bei, hatimaye mfanyabiashara huyo amefunguka 👇
-
"Ni kweli tunahitaji huduma zenu kwenye biashara zetu, lakini ifike point mziheshimu brands za wateja wenu na mahusiano yao na watu wengine, kuna maisha baada ya mitandao ya kijamii."
-
"Nimeshakuonya mara nyingi, nilikufungulia mpaka mashtaka ukatuma watu yakaisha, nasema mara ya mwisho nakuomba koma mara moja kunitaja au kutaja kampuni yetu “VUNJABEI” kwenye mambo yako." Ameandika Fred Vunja Bei kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Chanzo: capitaldigitaltanzania
La Kipanya bado hujalimaliza sasa umehamia kwa Mwingine. Hivi huna Washauri wakusaidie? Unakoelekea ni kubaya kuliko ulikotoka.
Yani inahitajika mdahalo kujua mtu fulani ni tajiri? Ni wazi hakuna tajiri kati yao…! Matajiri wahangaiki na midaharo!
Diamond huwa akipelekewa demand note na TRA anaanza kulia…! Diamond ni mpambanaji bado hajafika level ya kuwa tajiri