jaribu kunywa maji mengi angalau lita 3 hadi 4 kwa siku kisha fanya mazoezi ya kukimbia kila mara au badala ya kutembea kwa miguu nunua baiskeli endesha nyakati za jioni angalau maili 10 kwa siku.
Hii maili 10 ni kama saa1 ya mazoezi ya kawaida
Punguza mawazo(stress) kwani hili nalo linaweza kuchangia mwili wako kutofanya kazi vizuri na kuongeza tatizo lingine kama la kunuka mdomo,mkojo kuwa na harufu kali,kuzorota kwa afya yako n.k
Haya yote ni bure kabisa lakini pia unaweza nunua vikorombwezo vya dukani wakati unaendelea na dozi yako ya maji na mazoezi.
Pia kama una gym karibu yenye sauna au stimu rumu nenda kakae stimu rumu ni nzuri kwa kufungua matundu ya ngozi.
yaani hapa prince pepe amemamliza kila kitu. kunuka kwapa kunaendana na kua na jasho lenye harufu kali, au mkojo kutoa harufu kali. yote hii inatokana na kuzorota kwa mfumo wa taka mwili katika mwili wako. sasa kwasababu ya concentration ya hizo taka mwili ndo maana harufu inakuwa kali. ukitaka kuprove hii, angalia mkojo wako ni upi unakuwa na harufu zaidi, ule unaoelekea kwenye weupe au ule wa kahawia?! mkojo unavyozidi kuwa wa kahawia ndivyo unavyozidi kuwa na harufu.
so the same kwa jasho, unavyozidi kuwa na takamwili nyingi, concentration katika jasho inaongezeka na ndiyo na harufu inakuwa kali. asikwambie mtu!!! perfumes siyo dawa hata kidogo, dawa ni kubadili mfumo wa maisha yako, sasa zingatia mambo matatu yafuatayo
1. kunywa maji ya kutosha kwa siku, na usinywe maji mengi, zaidi ya nusu lita kwa mara moja!!!! hapana, kunywa walau glasi nane za maji sawa na lita mbili kwa siku, zigawe vizuri tu ili uhakikishe kuwa zinatimia kwa siku moja
2. fanya mazoezi ya kutosha yatakayo hakikisha unatoka jasho la kutosha ili taka mwili ziishe, kumbuka kwenye mfano wetu wa mkojo, kadri mkojo unavyokuwa clear ndivyo na harufu inavyopungua
3. angalia msosi unaotupia, vyakula vyenye asidi (uric acid) na jamii ya nyama husababisha taka mwili nyingi. ndo maana kwa mfano mkojo au jasho la mlevi linanuka vibaya sana. so kula matunda na mbogamboga za kutosha. hizi ni bora sana kuliko nyama na bia
after 3 to 5 dys lete majibu. trust me hii kitu ni nzuri na ya kweli, mi binafsi imenisaidia sana, na wengine nilowashauri wakazingatia imewafaa saana
akido