Pyaar
JF-Expert Member
- Feb 11, 2018
- 16,078
- 77,186
Amani ya Bwana iwe pamoja nanyi.
As-salaam Alaikum! Kwa ule upande wa pili.
Kumekucha! Na shughuli za utafutaji wa chochote kitu unaendelea.
Kwa upande wangu nimeamka hali si shwari sana kutokana na yaliyonikuta usiku wa manane (leo).
Baada ya mihangaiko ya jana kutwa nzima kama ilivyo kawaida kwa baadhi yetu kupumzika usiku uingiapo, ilikuwa mishale ya saa 5 usiku, nilipoelemewa na usingizi na kuamua kulala.
Ilipofika mida ya saa 8 usiku nikashtuka usingizini ili niende msalani, maana imekuwa kama ada kwangu kabla sijalala kunywa uji vikombe viwili vitatu [emoji5] .
Ile nafika mlango wa chooni kabla sijaufungua nikahisi nywele kunisimama ghafla, sikujali nikaendelea na kilichonipeleka.
Mara ghafla nikakumbuka kilichomtokea jamaa yake NORSHAD aliyechambwa kibabe na watu wasiojulikana.
Nilirudi kulala (muda huo ilikuwa saa 8:15). Hapa ndipo ziara yangu kupitia ndoto ilianza rasmi.
NDOTO
Sehemu ya kwanza
01.Niliuendea mlango kwa lengo la kuufunga ili nilale (usiku), lakini kabla sijafunga kitu chenye umbo kama kitoto hatua ya kimjusi (fetus) kikachomoka kutoka nje na kuingia ndani, kwa ujasiri nikakitoa nje, nikausukuma mlango kwa mara nyingine ili kuufunga mara kaingia mtoto wa miaka 7-8 hivi, kwa ubabe nikakisukuma kikaanguka nje. Baada ya kuona hivyo nikaanza kukemea kwa imani yangu lakini bahati mbaya sauti haikuweza kutoka.
Sehemu ya pili
02. Nikiwa natembea sijui wapi naelekea mara ghafla nikaivaa nyumba moja ina mbwa kama 7 hivi, wakaanza kunitisha kama wanataka kunifuata, nikaogopa nikaondoka zangu. Mara nikasikia sauti za hao mbwa kwa idadi yao wakiniambia "UMECHAFUKA MGONGONI" ([emoji28][emoji28] dah!) tena kwa pamoja kama wameambizana.
Bwana eeh! Nikapiga moyo konde kuwauliza "Nyie mmenionaje wakati ni usiku na hakuna mwanga"? Nikaambulia kuchekwa na hao mbwa.
Baada ya muda nikashtuka usingizini na kuuhisi mwili haupo kawaida. Shingo inauma, mwili kama umepigwa ganzi.
Mshana Jr., Humble African na wale magwiji waliobarikiwa kutafsiri ndoto karibuni.