Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwili wa mtu ambaye hajatambulika umekutwa pembezoni mwa barabara chini ya mti wa muembe katika Mtaa wa Mtakuja, Kata ya Malolo, Manispaa ya Tabora mkoani Tabora. Tukio hilo limeripotiwa baada ya wakazi wa eneo hilo kuona nzi wakiruka katika eneo husika.
Mkazi wa eneo hilo, Dorothy Fungamizi, amesema waligundua mwili huo baada ya mvua kunyesha, na kudai kuwa huenda kifo chake kilisababishwa na njaa.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mtakuja, Hamisi Ibrahim, amethibitisha tukio hilo huku akisema marehemu hakuwa mkazi wa eneo hilo.
Naye Diwani wa Kata ya Malolo, Bi. Zinduna Kambagwa, amesema marehemu alionekana mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Tabora, akiwa na ulemavu wa mkono mmoja. Amesema mwili huo tayari umechukuliwa na Jeshi la Polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete.