Mwili wa Joshua Mollel umewasili nchini Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,112
Reaction score
34,951

Mwili wa Mtanzania Joshua Mollel aliyeuawa na Hamas kuwasili leo kutoka Israel​


Maelezo ya picha,Mwili wa Mtanzania Joshua Mollel ukiagwa nchini Israel kabla ya kurudishwa Tanzania, aliuawa na Hamas katika shambulizi la oktoba 7.
Mwili wa Joshua Loitu Mollel, raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 21 aliyeuawa na Hamas wakati wa mauaji ya Oktoba 7, utawasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, ambapo utapokelewa na familia yake na mamlaka ya serikali.
Mapema jana, Ubalozi wa Tanzania nchini Israel ulifanya ibada ya katika mnara wa kumbukumbu wa Tel Aviv kabla ya kuondoka kwa mwili huo.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua.
Mollel alikuwa akifanya mafunzo ya kilimo kusini mwa Israel wakati watu wenye silaha wakiongozwa na Hamas waliposhambulia mnamo Oktoba 7, 2023.


Aliuawa huko Kibbutz Nahal Oz, na mwili wake baadaye ukachukuliwa na washambuliaji.
Israel imekabidhi miili ya Wapalestina 285 badala ya miili ya mateka 19 wa Israel iliyorejeshwa na Hamas, pamoja na ile ya mateka watatu wa kigeni, mmoja wa Thai, mmoja wa Nepal na mmoja wa Tanzania. chanzo.www.bbc.com
 
Hamas binaadam sana, kama nchi nyengine sio za kiislam, mwili ungalichomwa au kutupwa mtoni
Kiu binadamu kweli watuzzidi sana maana sisi tumekwenda kufukia miili ya watu kwenye makaburi ya pamoja na wengine inasemekana wamechomwa moto kupunguza jam. Laana haitawaacha watawala waliofanya haya!!
 
Ahsante sana Israel kwa kutufundisha utu. watanzania kwamba maisha yetu yanathamani kiasi gani katika hichi kipindi ambacho tunapitia kipindi kigumu. Ambacho serikali fake ya samia imeua maelfu ya raia wake na maiti kuzikatalia. Na wakati huo mabaki mtanzania mwenzetu mmoja Israel imebadilishana wapelestina hai karibia 300.
 
Unampongeza Isreal badala ya Hamas waliouhifadhi mwili zaidi mwaka? Wangaliopoteza Isreal angaliupata? Wewe kweli 0 brain
 
Hamas binaadam sana, kama nchi nyengine sio za kiislam, mwili ungalichomwa au kutupwa mtoni
Kama walivyotupwa watanzania waliuwawa oktoba 29. Nadhani polisi wa tanzania lazima walazimishwe kujua ubinadamu. Kosa halisahihishwi kwa kosa. Unafanya kosa la kuua halafu unasahihisha hilo kosa kwa kuwatupa kusikokujulikana maiti za waliouwawa ili usijulikane umefanya kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…