Nkarahacha
Member
- Oct 3, 2023
- 17
- 38
MWILI WA MTOTO ALIYEGONGWA NA GARI LA WENYEKITI WA UVCCM MKOA WA KAGERA FARIS BURUHAN WAZIKWA,SIMANZI KUBWA YATAWALA KWENYE FAMILIA YA MWANAFUNZI HUYO.
Mwili wa MWANAFUNZI Revina Kaumbya Leginard(9)wa darasa la tatu shule ya msingi Kamachumu B aliyegongwa na gari la Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera Faris Buruhan umezikwa Nyumbani kijiji Kanoni Kata Kamachumu wilaya ya Muleba.
Baba mzazi wa mtoto huyo anasema aliyefika siku ya Mazishi ni baba wa Dereva tu.
Mpaka sasa mamlaka husika hazijatoa taarifa yoyote kuhusiana na ajali hiyo na hata CCM wao wamekaa kimya juu ya mambo ya hovyo anayoyafanya Mwenyekiti huyo.
Watoto wengine wawili wapo mahututi katika hospitali ya rufaa Bukoba.
Ajali hii imetokea mapema wiki hii katika eneo la Kamachumu Senta wakati Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoa wa Kagera akitoka kuhitimisha ziara yake wilayani Muleba.
Ikumbukwe Faris Buruhan hivi karibuni alitoa kauli ya kuanza kuwapoteza watu wanaotukana mitandaoni huku akiwasihi polisi kwamba atakayepotezwa wasimtafute.
Nimekuwekea video kutoka kwenye familia ya MWANAFUNZI huyo.
Pia soma Kamachumu, Muleba: Msafara wa M/Kiti wa UVCCM Kagera waua watoto wawili