Mwili wa mtoto uliokutwa kwenye mashamba ya miwa Kilombero wazikwa

Mwili wa mtoto uliokutwa kwenye mashamba ya miwa Kilombero wazikwa

Mzee Rufiji

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2024
Posts
261
Reaction score
395
4:18 PM
538dc6d4ecc12956c42071a36e56f0c3
Mwili wa mtoto Rashmi Abdalah (5) ukiondolewa kwenye mashamba ya miwa wilayani Kilombero. Picha Happiness Mremi

Kilombero. Mwili wa mtoto Rashmi Abdallah (5), mkazi wa Kijiji cha Katurukila, wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, uliokutwa kwenye mashamba ya miwa wilayani humo, umezikwa katika makaburi ya familia kijijini hapo.

Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Akizungumza na Mwananchi Digital Jumapili Septemba 22, 2024, Mwenyekiti wa Kijiji cha Katurukila, Jela Meja amesema mtoto huyo na mama yake walifika kijijini hapo Agosti 7, 2024 kwa baba yake mkubwa, Joseph Nyoni, ili mtoto aanze masomo.

Hata hivyo, Septemba 12, 2024 mtoto huyo alitoweka nyumbani wakati akicheza na wenzake.

Meja amesema wazazi walitoa taarifa ofisi ya kitongoji cha Kondo baada ya kumtafuta bila mafanikio.
“Taarifa hizo zilipelekwa ofisi ya kijiji, ambapo walipiga mbiu ya mgambo na kuanza msako wa kumtafuta mtoto katika mashamba, mapori na vijiji jirani, lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda,” amesema.

Amesema Septemba 18, 2024 zikiwa zimepita siku sita tangu mtoto huyo apotee, walipata taarifa kuwa mwili wake umekutwa kwenye mashamba ya miwa yaliyokuwa yameungua moto ukiwa umeungua pia.

Mwenyekiti Meja alibainisha kuwa si tukio la kwanza la watu kutoweka katika eneo hilo, ambapo kuna mwanamke kutoka kijiji jirani aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha na bado hajapatikana mpaka sasa.

Kwa upande wake baba mkubwa wa Rashmi, Joseph Nyoni amesema mtoto huyo alikuja kijijini hapo kwa ajili ya masomo.

Alitoweka siku ya Jumapili, Septemba 12, wakati yeye akiwa kanisani. “Baada ya jitihada za awali za kumtafuta kushindikana, waliripoti tukio hilo kwa ofisi ya kijiji na kuendelea kumtafuta,” amesema.

Nyoni amesema Septemba 18, 2024 alipokea simu iliyoeleza kuwa mwili wa mtoto umepatikana katika mashamba ya miwa ya Kilombero, yakiwa yameungua.

“Niliutambua mwili wa mtoto kupitia kipande cha nguo ambacho kilikuwa kimeungua,” amesema.
Baba huyo ameiomba Serikali ifuatilie tukio hilo kwa kina na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika.
Amesema mtoto huyo alikuwa wa pekee kwa wazazi wake na baba yake mzazi alifariki baada ya mtoto huyo kuzaliwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema uchunguzi unaendelea.

Pia ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi wa tukio hilo.

©Mwananchi
 
Dah, dhulma ya kunyang'anywa uhai aliyofanyiwa Binti huyu inasikitisha sana!!

Umri kama huo, Hana baya lolote alitendalo au aliwazalo kwa mtu zaidi ya kucheza tu wenzake wamemuulia nini'?!!!!!!!

Mungu wa mbinguni lipa vikali hili.
 
Ni vigumu kuhukumu moja kwa moja kuwa nini kimetoa uhai wa binti mdogo wa miaka mitano na mwili wake kukutwa katikati ya mashamba makubwa ya miwa ambapo na pengine kwa umri wake ni aghalabu kufika huko.....

Fikra zinakusuma kuwa huenda ameuwawa na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa huko lakini bado unajawa na maswali kuwa binti mdogo au mtoto mdogo wa umri huo ana heka heka gani kwenye ulimwengu huu dhidi ya walimwengu kiasi cha kuwaudhi mpaka kufikia kuona kuwa adhabu pekee ni kumuua tena kifo cha kikatili......

Mawazo ya karibu yanagota kwenye ubakaji kwa asilimia kubwa sana kutokana na mazingira ya tukio na mwenendo au kushamiri kwa wingi wa matukio hayo.....nje ya roho ya kishetani na kinyama mwanaume mtu hana kinachomvutia kwenye maungo ya mtoto wa miaka mitano.......

Kwa uzoefu tulionao kwenye utendaji kazi wa jeshi letu la polisi inawezekana likabakia kuwa FUMBO la milele kuhusu nini kimemkuta mtoto huyo......

Hatuna budi kumuomba mola wetu mlezi amlaze mahala Pema peponi.....
 
Back
Top Bottom