Mwimbaji Chaz Baba nusura amuue mkewe, ampiga na kitu kizito kichwani mpaka mke kuzimia

Nyasamaki

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
1,055
Reaction score
595






PREZIDAA wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel Mbwana ‘Chaz Baba' anadaiwa nusura amtoe roho mkewe wa ndoa, Rehema Sospeter Marwa baada ya kumpiga na kitu kizito kichwani mpaka kushonwa nyuzi ishirini.

MANENO YA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo karibu na wanafamilia hao (jina limehifadhiwa), usiku wa Alhamisi iliyopita, kikiwa maeneo ya Kinondoni jijini Dar kilishuhudia ugomvi huo baada ya kwenda kuangalia nani anamshushia kipondo mwenzake.

Chanzo kilisema baada ya kufika, ndipo kiligundua kuwa, mwanamuziki huyo ndiye aliyekuwa akimpa kipondo mke wake.

"Dah! Kiukweli kile si kipigo cha kumpiga mke, hasira bwana ni kitu cha ajabu sana. Chaz anatakiwa kujiangalia sana," kilidai chanzo hicho.

MKE AFUNGUKA ‘EI TU ZEDI'
Baada ya taarifa hiyo, juzi Ijumaa Wikienda lilimtafuta mwanamke huyo ili aeleze nini kilitokea hadi mumewe kutaka kumkatishia maisha."Nakumbuka siku ya tukio nilikuwa supermarket maeneo ya Mwananyamala A (jijini Dar) nikinunua unga wa ulezi wa mtoto, ghafla Chaz alitokea, akaniamuru niingie kwenye gari alilokuwemo, tukaondoka kuelekea nyumbani.

"Tulipofika maeneo ya Kinondoni, pale Meridian ndipo niliposhtukia naanza kupigwa. Nakumbuka nilipigwa hadi nikaishiwa nguvu mpaka akatokea rafiki wa Chaz, Hassan Kisanora na kuniokoa, nikakimbilia nyumbani," alisema mwanamke huyo.

CHAZ ATOWEKA, ARUDI NA SAMAKI MKUBWA
Akiendelea kuzungumza, mke huyo alisema: "Siku hiyo Chaz aliondoka na hakurudi nyumbani mpaka alfajiri. Aliporudi aliniambia amekuja na samaki mkubwa, yuko kwenye friji huku akisahau kuwa amenikosea na anatakiwa kuniomba msamaha.

"Sikumjibu, ndipo alipochukua kitu kizito na kunipiga nacho kichwani, baada ya hapo damu nyingi zikaanza kunitoka hadi puani, niliishiwa nguvu na kupoteza fahamu."
"Nilipokuja kuzinduka nilikuwa hospitali kwa Dk. Mvungi, Kinondoni. Licha ya kwamba nampenda sana lakini alitaka kuniua, hata sijui kisa."

MADAI YA KUSHANGAZA; NDANI YA MIEZI TISA KICHAPO MARA 16
Katika kuweka mambo zaidi hadharani, mwanamke huyo aliyebahatika kupata mtoto mmoja na mumewe, alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, tangu afunge ndoa na Chaz miezi tisa iliyopita, ameshachezea kichapo mara kumi na sita hivyo amechoka kufanywa ngoma."Nimechoka kufanywa ngoma na Chaz, ndoa ina miezi tisa tu nishapigwa mara kumi na sita kati ya hizo nimezimia mara saba kama vipi bora afanye utaratibu anirudishe kwetu," alimalizia kusema.

CHAZ BABA, IJUMAA WIKIENDA
Baada ya kupata maelezo ya mke, Ijumaa Wikienda lilimsaka kwa njia ya simu Chaz mwenyewe ili azungumzie ishu hiyo ya mkewe kudai alimpiga ambapo alipopatikana alifunguka hivi:

"Ni wivu tu kaka! Unajua mke wangu ana wivu mkali sana, alianza kunipiga yeye mimi ndiyo nikamrudishia, hakukuwa na sababu nyingine yoyote zaidi ya wivu," alisema Chaz bila kufafanua.
GP

 
Umepigwa mara kibao na ushazimia mara 7, but still upo tu umekomaa na ndoa. Una uhakika gani kama next time utakavyopigwa uta-survive? Hata kama wewe ndo umekosea labda, ndo upigwe hadi na kitu kizito kichwani? What if ungekufa? Hicho kichapo cha kwenye picha ni kwa ajili ya mke au mwizi?
Jamani wanawake tusilete utani na maisha. Usichukulie maisha kama ni kitu simple hivyo, kwamba utapigwa but utakuwa tu ok. Kesho utapigwa hadi ufe then tubaki tunalia tu afu tutakusahau tu baadaye. Na wewe charles kama mtu kakushinda si umuache tu. Utamuua mtoto wa watu afu uishie jela mfyuuuuuuuuu
 
Hivi sheria za Tanzania zinasemaje? Maana ninavyojua mimi nchi nyingine wanawake wanalindwa sana na sheria.
 

Badala ya kutoka Nduki kangangania tu kisa na yeye KAOLEWA MJINI Uwiii !
 
Uvumilivu wa kichapo kwenye ndoa nimeapa sitakubali ukijaribu kunipiga hata kibao we loose each other kama unapesa jua natafuta namna ya kukufilisi ndiyo nisepe
 
Wewe huoni ni ujiko kuitwa mke wa Chalz Baba?

Halafu bado kuna mizembe inawasema wadada over 30 ambao hawajaolewa, sasa hii ni ndoa au gereza?

Kwa huyu, hiyo siyo ndoa ila ni kaburi lake. Na kama kuitwa mrs charles ni sifa, basi hizo sifa zitampeleka kaburini.
Hamna ndoa isiyo na matatizo 100%, but kuliko kuwa kwenye gereza la ndoa kama hii, basi ni bora tu mtu uishi peke yako khaaa
 
dada anataka kufia mikononi kwa mumewe kwa kichapo
 
Chaz baba umechemka!mwanamke hapigwi ngumi,mwanamke anapigwa na u.b.o.o
 
dada anataka kufia mikononi kwa mumewe kwa kichapo

Kuna wanawake hawajipendi kabisa yaani anajitoa muhanga maisha yako kisa mume kwa kipi kikubwaaa? Kupigwa hadi kuzimia alafu yupo tu anang'ang'ania hata ingekua jamaa ana pumbu za dhahabu lol
 
Tatizo nii...

Sikujua ya kwamba wewe ni msaliti,umezoea kugawa gawa kwa kila mutu eeeeh....eti kwa sababu ni mwanamke mzuri hutaki kutuliaaa.......
 
kisa cha kumpiga mwanamke ivo ni nn? huyo dada nahisi bado ajatambua haki zake.
 
Aaaaaaa kumbe mke mwenyewe ni MKURIA :what:
Kawaida yao hw bila kichapo huwa wanadai hawapendwi

By: tafiti Hakinifu%
 
Aisee ndio kupiga gani huko????mi naachika kabisaaa
 
Kuna wanawake hawajipendi kabisa yaani anajitoa muhanga maisha yako kisa mume kwa kipi kikubwaaa? Kupigwa hadi kuzimia alafu yupo tu anang'ang'ania hata ingekua jamaa ana pumbu za dhahabu lol

Hayo Maneno ni wewe farkhina umetoa, au kuna mtu kavamia account yako?
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…