Mwimbaji Qaswida aandaa tamasha Morogoro kusaidia Yatima

Mwimbaji Qaswida aandaa tamasha Morogoro kusaidia Yatima

DodomaTZ

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
84
Reaction score
118
0e5dcc56-ab6b-461e-9ba6-04bfdb76a3d3.jpg
Mwimbaji Qaswida maarufu hapa nchini, Abdulhamid Fannan ameandaa tamasha la kusaidia Yatima na wengine wenye uhitaji litakalofanyika Oktoba 5 mkoani Morogoro.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Fannan alisema katika tamasha hilo atawashirikisha waimbaji mashuhuri kutoka nje ya Tanzania akiwemo Hassan Mugisha (Burundi) na Arash Ajan (Kenya).
Kwa hapa nchini, waimbaji Hafidhi Ngozi aliyewahi kutamba na qaswida ya maalbino, wengine ni Arafa Hussein, Said Mussa Huraira, Arafa Abdallah, Ally Ismail na wengine wengi.

Fannan alisema kwa sababu ya uhitaji huo, kila mwaka hufanya tukio kama hilo kwani ndio agizo la Mwenyeezi Mungu kuwasaidia waja wake wenye uhitaji.

Aidha Fannan ambaye anaongoza kundi la Daarul Swaut Crew amewaomba wakazi wa Morogoro na maeneo ya karibu kuhudhuria kws wingi katika tamasha hilo ambako watashuhudia matukio mengi likiwemo la umahiri wa kuimba Qaswida.

Fannan katika mojawapo ya matamasha yake, aliwahi kushirikiana na mwanamuziki nguli hapa nchini, Ali Kiba katika baadhi ya matamasha ya kusaidia Yatima mkoani Kigoma.
 
Back
Top Bottom