Mwimbaji Shakira kufungwa jela kisa kutolipa kodi

Mwimbaji Shakira kufungwa jela kisa kutolipa kodi

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Shakira2.jpg

Mwimbaji staa tokea nchini Colombia, Shakira anaweza kufungwa jela kutokana na kosa ambalo limekuwa likiwapeleka mastaa wengi Mahakamani nchini Hispania la kushindwa kulipa kodi.

Mamlaka ya kukusanya kodi nchini Uhispania imemtaka Shakira kupeleka rekodi ya fedha zake kuanzia 2011-2014 kufuatia habari za Shakira kukwepa kulipa kodi mwaka jana.

Habari hizo ziliandikwa katika magazeti ya Panama na taarifa katika gazeti la “La Vanguardia” la Catalonia, ofisi ya kulipa kodi ya Catalonia imesema kuwa Shakira aliishi Uhispania katika kipindi cha kati ya miaka 2011-2014 na anatakiwa kulipa kodi.

Shakira mwenye umri wa miaka 40 ana watoto wawili na mchezaji mpira maarufu wa Uhispania Gerard Pique.

Muungwana
 
Hawa jamaa inamaana mifumo yao ya kodi ni dhaifu kama bongland au? Kwanini kusiwe utaratibu mtu ajulishwe na akatwe kodi akifika tu bila kusubiri miaka 2 au 3 kupita? Tushawachona nao wapigaji tu
 
Kuna mtu aliwahi nidokeza kuwa Spain maisha ni magumu sana kiasi kwamba hata watu wake ni wabahili kupita kiasi. Kwa wale walio kwenye sekta ya utalii wanalifahamu hili kwani hata watalii kutoka huko ni wachache sana ukilinganisha na mataifa mengine ya Ulaya. Ajira pia ni ngumu sana kwa hawa watu kama vile bongo land ,kati ya miaka ya hivi karibuni ilishawahi kutokea wachezaji wa timu ya Real Sociedad inayoshiliki La Liga kugoma baada ya kutolipwa mishahara kwa muda mrefu. So hata wao wanakamua kodi si mchezo mchezo ili kukidhi na mahitaji ya jamii yao.
 
View attachment 683495
Mwimbaji staa tokea nchini Colombia, Shakira anaweza kufungwa jela kutokana na kosa ambalo limekuwa likiwapeleka mastaa wengi Mahakamani nchini Hispania la kushindwa kulipa kodi.

Mamlaka ya kukusanya kodi nchini Uhispania imemtaka Shakira kupeleka rekodi ya fedha zake kuanzia 2011-2014 kufuatia habari za Shakira kukwepa kulipa kodi mwaka jana.

Habari hizo ziliandikwa katika magazeti ya Panama na taarifa katika gazeti la “La Vanguardia” la Catalonia, ofisi ya kulipa kodi ya Catalonia imesema kuwa Shakira aliishi Uhispania katika kipindi cha kati ya miaka 2011-2014 na anatakiwa kulipa kodi.

Shakira mwenye umri wa miaka 40 ana watoto wawili na mchezaji mpira maarufu wa Uhispania Gerard Pique.

Muungwana

Ingekuwa Bongo hiyo ungesikia matakataka yangekuja na misemo sijui visasi, mara yana mwisho sijui malipo hapa hapa watatatea utafikiri huyo mhalifu huwa anatumia hela zake na wao!
 
Back
Top Bottom