Mwina Kaduguda na wenzako, kwanini hamtaki kuvaa jezi za M Bet, mnatufundisha nini sisi mashabiki

Mwina Kaduguda na wenzako, kwanini hamtaki kuvaa jezi za M Bet, mnatufundisha nini sisi mashabiki

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Nimeangalia gemu ya juzi ya Simba vs kagera sugar nimemuona mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Simba anayewakilisha wanachama Bw.Mwina Seif Kaduguda akiwa amevalia jezi ya Simba ikiwa na nembo ya Sportpesa.
Kiukweli nimesikitika sana, Simba imeingia mkataba na M bet, mkataba mnono kuliko ule Yanga vs Sportpesa, lkn bado baadhi ya viongozi wa Simba wanavaa jezi zenye nembo ya Sportpesa, hii maana yake ni nini, je wanasaliti udhamini wa M bet, je hawakubaliani na mkataba huo, je Kaduguda hana uwezo wa kununua jezi mpya ya M bet, je kitendo cha Kaduguda na wenzake kuvaa jezi za sportpesa ilhali sasa tuko na M bet kinaashiria nini, je viongozi wetu wanatufundisha nini, hawa watu kweli wako wamoja ama wako kwa maslahi binafsi.

Nawaomba mashabiki wa Simba, ni usaliti mkubwa sana kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wa yanga, sisi mdhamini wetu ni M bet, mtu yeyote anayevaa jezi za sportpesa huyo sio mwenzetu, huyo ni yanga.
 
Kaduguda ni tatizo Simba nimesoma makala yake kwenye gazeti la msimbazi wiki iliyopita anasema Simba Haina kiungo mkabaji na mshambuliaji lakini anapoandika hivyo anasahau yeye ni kiongozi na yupo kwenye bodi hivi ameshindwa nini kuongeza kwenye bodi, kama ameongea na hasikilizwi si Bora ajiuzuru kuliko kutuletea majungu yake
 
Huyu Mzee ni kimeo tu hapo Simba anaabudu sana ushirikina
 
Simba ipo vizuri tatizo mo yule ni wa kufukuzaa simba pale
Kumbuka huyo Mo ndiye ameifanya Simba iwe vizuri kama GSM alivyoifanya Yanga yenu iwe ilivyo sasa. Bila hela hakuna mpira. Nyie jaribuni kumfukuza GSM muone moto utakavyowawakia. Masikini hana kiapo
 
Back
Top Bottom