Mwina Kaduguda tafadhali pokea Simu yako tafadhali ili Ufe kwa Kujitoa Mhanga na Simba SC Kesho tushide kwani mpaka Saa 7 leo Yanga 3 na Simba 0

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Mtakaonichukia ( hasa Watu wa Simba SC ) mtanisamehe ila nisiwafiche Watu ( Kamati ya Ufundi na Utamaduni ) wanahangaika mno na mpaka Saa 7 Mchana leo bado Mtaalam anasema Yanga SC 3 na Simba SC 0 Kesho Mkapa Stadium.

Na sehemu ambayo Yanga SC wametuweza Simba SC ni katika Suala la muda wa Mchezo ambao ni Saa 11 jioni muda ambao Kinyota ( Kinujumu ) ni mzuri kwa Simba SC hali inayopelekea Mtaalam wetu kuwa na wakati mgumu.


Mjumbe Mmoja aliyeko katika Kamati hiyo amenidokeza MINOCYCLINE kuwa Suluhu pekee kwa Simba SC kubadili Upepo ni kwa Kutoa Kafara ya ama Mtu Mmoja ( tena Maarufu na awe Kiongozi ndani ya Klabu ) au Watu zaidi ya Watano kitu ambacho mpaka sasa Kimewachanganya huku Mtaalam akiwaambia Yanga SC 3 na Simba SC 0 Kesho.

Binafsi kama MINOCYCLINE nimejitahidi Kumtafuta Mwina Seif Kaduguda ( Simba wa Yuda ) kwa namba zake zote Tatu, kwa Mkewe Kwake Mbagala na kwa Rafiki yake wa karibu ( Kiongozi Serikalini na CCM ) ili ajitoe Mhanga ( Afe ) kama ambavyo alishaahidi na atuokoe Simba SC Kesho kwa Aibu hii ya Kufungwa hizo Goli 3 kwa 0 ambazo mpaka sasa zinasomeka, zimeng'ang'ania na wala hazina mpango wa Kufutika.

Namalizia kwa Kusisitiza kuwa kama upepo utabadilika au Mtaalam atapambana kuanzia Jioni hii, Usiku hadi Kesho ili Simba SC yetu ishinde sawa na MINOCYCLINE nitafurahi kupita Maelezo, ila kwa mujibu wa Watu wa Kamati husika walioko kwa Mtaalam wanasema Yanga SC watashinda Goli 3 kwa 0 ya Simba SC.

Usiku nitatoa Siri aliyosema huyo Mtaalam kumhusu Mshambuliaji hatari wa Yanga SC Fiston Kalala Mayele na kwanini anafunga sana, ameshindikana na kila akifunga tu Goli Moja huwa analazimisha kutoka Nje tena muda mwingine akijifanya Kaumia / Ameumia.

Ukiutaka huu Uhondo ambao nitaufungulia Uzi wake kuanzia Saa 4 Kamili hadi Saa 5 na dakika 59 Usiku wa Leo usibanduke hapa Jamiiforums na endelea tu kuwepo hapa Jamiiforums kila wakati na kamwe ID hii ya MINOCYCLINE usikae nayo mbali na hata Unaichukia Wewe ivumilie tu kwani imesheheni Taarifa za Jikoni kutoka Yanga SC na Simba SC.
 
Mtakaonichukia ( hasa Watu wa Simba SC ) mtanisamehe ila nisiwafiche Watu ( Kamati ya Ufundi na Utamaduni ) wanahangaika mno na mpaka Saa 7 Mchana leo bado Mtaalam anasema Yanga SC 3 na Simba SC 0 Kesho Mkapa Stadium.
Huyo ni mtaalamu wa mchongo.
 
Genta kama Genta.

Yeye mechi za simba au yanga kabla haijachezwa anakua na matokeo tayari😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…