LGE2024 Mwingine apiga magoti! Chagueni CCM izidi kuwaletea maendeleo! Bado kuruka tu kama Wamasai!

LGE2024 Mwingine apiga magoti! Chagueni CCM izidi kuwaletea maendeleo! Bado kuruka tu kama Wamasai!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Safari hii kweli mambo magumu kwa CCM, mbinu za kijasusi zote zinatumika kuomba kura, bado kugeuza macho tu kama akina Zuchu :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Screenshot 2024-11-24 211002.png

Kupata nyuzi za kimkoa Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mbunge wa Vijana Taifa, Ngw’asi Kamani amewaomba Wananchi kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi kuwaletea maendeleo katika miaka mitano inayokuja ya uongozi wa Serikali za Mitaa 2024-2029.

Screenshot 2024-11-24 211013.png

Kamani ameyasema hayo Wilayani Magu katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa akizifanya Kijiji kwa Kijiji, Mtaa kwa Mtaa, Nyumba kwa Nyumba na kuwaomba wananchi kuwachagua wagombea wa CCM.

Kwa vimbwanga na vituko vingine kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ruka hapa: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Screenshot 2024-11-24 211027.png

“Nawashukuru kwa kuipa CCM ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa 2019 na 2020, naomba tujitokeze kwa wingi tarehe 27 Novemba 2024 mkapige kura za NDIO kwa CCM ili kumrahisishia Rais Samia kuleta maendeleo katika vijiji na vitongoji vyetu.
 
Back
Top Bottom