Aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC Mwinyi Zahera ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi kuu ya NBC Tanzania bara kwa mkataba wa miezi 6 mpaka mwisho wa msimu.
Hivi sasa Mwinyi Zahera anatambuliswa kwa wachezaji wa Maafande hao wa Polisi Tanzania.
Mimi nilijua tu kwa kitendo kile kuisema Yanga kwenye media huku akionekana kupaka mchanga kibarua cha Nabi nikajua huyu anatafuta ulaji aidha Yanga au anajipigia chapuo sehemu nyingine.
Maana wangempa mkataba mrefu; basi kwenye usajili wa dirisha dogo la January, lazima angemrudisha tena nchini yule mshambuliaji wake butu Papaa David Molinga "Falcao"