Aliyekuwa kocha wa Zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ametangazwa na team ya Gwambina fc kuwa mkurugenzi mkuu wa ufundi wa team hiyo. Gwambina inakuwa team ya kwanza Tanzania kuwa na cheo Cha mkurugenzi mkuu wa ufundi, mfumo huu Ni mahususi Sana bara la ulaya mfano mzuri pale Chelsea mkurugenzi mkuu wa ufundi Ni Marina Granovskaia, ukienda Arsenal Wana edu ukienda Bayern Munich Wana Hasan Salihamidzic, Dortmund Wana Michael Zorc.