Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amesema malengo yao msimu huu hayakuwa kushiriki michuano ya Kimataifa na hata kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho
Zahera ameyasema hayo mara baada ya kipigo cha jana cha goli 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Azam Sports Federation Cup(ASFC) uliofanyika katika Uwanja wa Samora mjini Iringa
Pia, amedai kwenye ligi malengo yao hayakuwa kubeba ubingwa lakini baada ya kuwa wanacheza na wanashinda wakaamini kuwa wanaweza kubeba ubingwa
Kocha huyo ameongeza kuwa hawana cha kupoteza kipindi hiki na sasa wanajipanga kwa msimu ujao baada ya kushindwa kuwa mabingwa wa kombe na ASFC