Mwinyi Zahera: Narejea Tanzania kuchukua malimbikizo yangu ya fedha kwa Yanga

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kesho Jumatano alfajiri anarudi Tanzania kufuata malimbikizo ya madeni yake kwa uongozi wa klabu hiyo

Zahera alifungashiwa virago vyake baada ya kushindwa kufikia malengo ya klabu hiyo ambapo nafasi yake inakaimiwa na Bonface Mkwasa

Zahera amesema hakuna mahala aliposaini barua ya kutimuliwa Yanga na hajalipwa malimbikizo ya madai yake hivyo anarudi kufuata

"Nitafika Tanzania saa 8 alfajili kesho Yanga hawajanilipa fedha yangu na bado sijasaini barua ya kuvunja mkataba na klabu hiyo,"

"Siwezi kuendelea kukaa huku nikiwa bado sijamalizana na Yanga narudi tena Tanzania kwaajili ya kudai fedha zangu na kusaini hiyo barua ya kuvunja mkataba kama wao wanavyotaka," alisema.
 
Sasa walikuwa wanasubiri nini kumpa barua
 
Mwinyi Zahera a.k.a Pilipili! Viongozi wamalizane naye tu mapema ili tupumue.
 
Awahi media tour maana story zake waandishi wanasubilia kwa hamu cos hawana ubunifu mwingine
 
Sijasaini barua ya kutimuliwa so umetoroka kazini bila ridhaaa ya mwajiriii
 
Tabu ipo pale pale[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Mdhamini kasema
 
Naona hawajampa barua maana anadai hela nyingi wakaona wakimpa barua atawadai heri wampotezee kwanza
Yanga waangalie asije akakamata ki Yutong chao kama mzungu wa ndege zetu anavyosumbua.
 
Yule Kocha mvua vipensi Mwinyi Zahera ameahidi kufika kesho kuja kusaini mkataba wa ukatishwaji kuifundisha Yanga.Pamoja ni hilo pia kuja kulipa fedha zake za kuvunja mkataba kuliko fanywa na Klabu ya Yanga.Shime WanaYanga tujitokeze na Vipensi vyetu kumpokea Mwinyi Zahera.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…