Mwinyi Zahera ni msemaji wa yanga au kocha?

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Wadau naomba mnafahamishe juu ya kazi sahihi ya Mwinyi Zahera je ni Msemaji wa Yanga au ni Kocha wa Yanga? Napata taabu kumtofautisha na Msemaji wa Simba Haji Manara kwani kila siku Mwinyi Zahera lazima atokee kwenye magazeti ,radio na TV kama Haji Manara .
 
Kocha wa timu anaweza kuwa msemaje wa timu hasa kwenye maswala yanayo husiana na uchezaji wa timu (mbinu, wachezaji, na ufundi) hata timu za ulaya maswala yote yanahusu ndani ya uwanja anaongea kocha. Kwenye ishu ya Zahera kuonekana sana kwenye magazeti na tv umemlinganisha na Haji Manara, kwa mtazamo wangu naona kwavile tu waandishi wengi wa habari wanapenda kumuhoji. Je mfano ungelikuwa wewe ni kocha halafu kila wakati waandishi wa habari wanakufuata kukuuliza uliza maswali kuhusu mchezo wako au kuhusu uwezo wa wachezaji wako je ungekaa tu kimya?
 
Ni Tanzania pekee unakuta msemaji wa timu anaongelea technical issues, hayo ni mambo ya kocha.
 
Si uende ukamuulize mwenyewe! Au unamuogopa?
 
Jina lakuuzia magazeti hilo, wakati mwingine huloshwa maneno I'll biashara iende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…