Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Mwisho wa mwaka huu kila mtu anapambana kutimiza majukumu aliyoyapanga mwanzoni mwa mwaka.
Nimekutana na "special hire" zikiwa na maiti toka wiki iliyopita huko njiani, kama zote, pamoja na zile gari za kubebea maiti.
Kiufupi, popote ulipo kaa karibu na Mungu. Mwisho wa mwaka unakuwaga mgumu na mkatili sana. Usishangae, hata kama hujawahi kwenda bar, anatokea pepo anarusha chupa kwa mwingine, lakini inakupata wewe.
Miaka kadhaa iliyopita, pale Rainbow mbele kuna bar, tulikuwa tunakaribia kumaliza mwaka. Tunaangalia mpira, wakaja vijana kadhaa wakachukua meza kadhaa — mashabiki wa Man U. Wakaja mashabiki wa Chelsea, wakachukua meza zao kadhaa na kujipanga.
Mpira umefika dakika ya 84, Chelsea anaongoza. Jamaa wa Man U anamwambia, "Tunashinda hii mechi, na tukishinda nakupiga bastola." Wale wenye CC tukashtuka, tukasema, mmh, unaweza kuwa utani lakini jamaa ana moto kweli. Mshabiki wa Chelsea akamwambia, "Mkishinda, niue!"
Tukasogea karibu na geti la kutokea. Dakika ya 90, Man U karudisha. Dakika ya 94, Man U kaweka kitu. Oooh, wenye BB tukatoka kabisa nje.
Mpira umeisha, tunasikia kelele za watu: "Kauaaa! Kauaaa!" na mlio wa bastola.
Jihadhari sana na sehemu za mkusanyiko mwisho wa mwaka. Ukiamka, jitengeneze njia na Mungu wako. Ukirudi salama, ongea, sema na Mungu wako, mwambie: "Ahsante kwa kunirudisha na kunitunza salama."
Good night.