Mwisho wa kutumia passport za kusafiria za zamani ni tarehe 31/Jan/2020

Mwisho wa kutumia passport za kusafiria za zamani ni tarehe 31/Jan/2020

kasulavenance

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2020
Posts
759
Reaction score
914
Mambo yamekuwa mambo Tanzania. Wakati bado tunasumbuliwa na NIDA na usajili wa line mpya kwa wale mliokuwa na passport za kusafiria mjue kuwa mwisho wake wa kutumia hati hizi za kusafiria ni kesho kutwa.

Inabidi kuanza zoezi jingine la kwenda Uhamiaji. Na shida inakuja pale unapoenda na kitambulisho cha taifa bado wanakuambia kalete barua toka mwenyekiti, cheti cha kuzaliwa nk.
 
kitambulisho cha Nida kina tosha kuchukua Passport uhamiaji acheni maswali zaidi kila kitu kiko kwenye kitambulisho cha Nida

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Tunge pata muhusika uhamiaji atupe abcd ya nn kinafanyika kama m2 ana kitambulisho cha taifa nida ikiwa ange hitaji passport ila haya mambo bhana dah!
 
Uhamiaji ukiwa unahitaji cheti cha bibi wa muombaji passport. Kwanza wewe onyesha cha bibi yako ili kumridhisha muombaji akione ndipo umuombe na yeye. nyie wote hamna mwenye cheti cha bibi yake wala babu yenu uhamiaji wengine sio raia wamejipenyeza tu serikalini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunge pata muhusika uhamiaji atupe abcd ya nn kinafanyika kama m2 ana kitambulisho cha taifa nida ikiwa ange hitaji passport ila haya mambo bhana dah!
Kama Mtu Anayo Namba Anaingia Kwenye Tovuti yao Anajaza form Upya Kama Mtu ambaye hana Tofautii Ipo sehemu ya kujaza Taarifa za Zamanii za Passport(Namba ya Passport, Sehemu ilipotolewa na Mwaka) huko Online utalipia 20K kwaajili ya hiyo form Kama Ada ya awali

Viambata Ni Muhimuu mfano Barua ya Mtendaji cheti/Affidavit n.k ukishawapelekea Utafanya malipo130K Na Kusubirii Sasa Passport Mpya Ya kielektroniki
 
20k means 20000 or 200000!!? Gharama ya hili zoezi zima mpaka unapata passport inachukua kiasi gani
 
Kama nina passport ya zamani nipo nje ya nchi, pindi nitakapotaka kurudi Tz itakuwaje? Nitarudishwa nilikotoka au? Ufafanuzi kidogo katika hili.
 
Gharama ya passport ni Tshs 150,000, kuna sehemu kwenye form yakuombea passport lazima a sign wakili hapa unalipigia kati ya 10,000 hadi 20,000

Kuna kutengeneza affidavit ya mzazi,kama alishafariki, hapa napo sio chini ya 20,000 kulipa kwa wakili... So gharama nzima hadi kupata passport andaa Tshs 200,000/=

Hapa hujaweka gharama zako binafisi,chakula,maji, maana ukienda pale unakata siku nzima (usafiri public au private),

Sent using Jamii Forums mobile app
Na nimesikia wanahitaji na vyeti pia vya shule original km cha form 4 na six kama sikusoma kuna ulazima gani?
 
Passport unaweza kubadilisha hata ukiwa nje ya nchi. Nenda ubalozi wa Tanzania kwenye hiyo nchi au kama hiyo nchi hakuna ubalozi wa TZ tafuta ubalozi iliyo karibu
Kama nina passport ya zamani nipo nje ya nchi, pindi nitakapotaka kurudi Tz itakuwaje? Nitarudishwa nilikotoka au? Ufafanuzi kidogo katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Passport unaweza kubadilisha hata ukiwa nje ya nchi. Nenda ubalozi wa Tanzania kwenye hiyo nchi au kama hiyo nchi hakuna ubalozi wa TZ tafuta ubalozi iliyo karibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni sawa, swali langu ni kwamba kama sitobadilisha nikaamua kuitumia hii ya zamani ninaweza kutoruhusiwa kusafiri kwenda Tz?
 
Back
Top Bottom