Mwisho wa zama za jirani yetu bwana Raila Odinga

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Hatimaye, zama za mbabe wa siasa za jirani zetu pale Kenya bwana Raila Odinga, dalili zote zinaashilia zi-ukingoni.

Kwa namna Rais Ruto anavyotaka kushughulika na mwamba yule, hakika, ni suala la mda kwa aina ya siasa alizozizoea kufanya ili matakwa yake yatimizwe-kwa msimamo wa Dk Ruto kutokutaka hayo yatimizwe, hakika, zama za Raila zinaenda kutamatishwa rasmi.

Raila, alizoea kila baada ya kushindwa uchaguzi, huanzisha vurugu ili aweze kumsababishia ubabaifu aliye shika hatamu, aweze kumwita wakae mezani na wagawane madaraka kwa kile kilichozoea kuitwa maridhiano ya hongo. Jambo hilo Dk Ruto, amelikataa!

Bwana Odinga, hivi karibuni, ameendeleza desturi ileile huenda kwa matarajio yaleyale ya yeye kutaka apewe hongo ya hand-shake na ionekane waliopo madarakani, wanamwabudu.

Lakini, kwa namna Ruto na msaidizi wake walivyo shikilia msimamo wao wa abadani hakutakuwa na hand-shake na Odinga, ni wazi zama za Raila zinaelekea kukoma.

Pamoja na rabsha za hapa na pale za maandamano ya hivi karibuni, lakini, zipo dalili Wakenya watamchoka Raila kwa wao kutokuona Serikali ya Ruto kubabaishwa na wanachokifanya na kushikiria kiburi na ndiposa wataona bora waendelee na kutafuta shilingi ya kuwafanya wapate chochote kitu na ndipo anguko la Raila litajiri/li.

Nionavyo, zama za Raila zipo ukingoni.
 
Mzee huyu apumzike tu siasani, atasababisha mafala wengi wanaoandamana kuuwawa kwenye ghasia. Mafala ni wajinga wanajitosa kuandamana, hayo maandamano wangemuachia huyo baba na wenzake akina martha karua na kolonzo waandamane front line. Hivi UN na AU wamekosa kazi za kumpa huyu baba aache kenya itulie? Wampe hata awe mjumbe wa amani huko sudan akatulize ghasia za huko
 
Ukanda wa afrika mashariki muda huu ingekuwa moto unawaka kila nchi. Tanzania nako kungekuwa na maandamano makali kupinga dp world ule mkataba wao, watz sio nyumbu wa kuandamana, hawataki kupambana na polisi wao, wamekaa kimya wakijilalamikia na kupinga gizani. Fujo za nini? Kenya ijufunze kwa tanzania kuacha maandamano yenye hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…