Elections 2010 Mwita Waitara Mwikwabe ashinda kura za maoni Tarime


Are you serious Kasyabone?
 
Ni kweli kabisa wenzangu wa Tarime msimtegemee Mwita Mwikwabe kuwaletea maendeleo.
Jamaa Bonge la Binafsi, mimi tumemaliza nae UDSM mwaka 2006 aliwahi kuwa Rais wa DARUSO aliyokuwa anafanya hayakutegemewa na waliomchagua.
Anyway pengine kabadilika jaribuni kumpa kama hakuna mwingine.
 

ni hopeless kweli-kweli na hafai!
 
hafai kabisa huyo jamaa, mimi mwaka 2006 nilikuwa mmoja wa mawaziri wa serikali yake-Jamaa hela yote alikuwa anakula kwa kushirikiana na waziri wa fedha na waziri. Tunapanga budget na hela yote anakula yeye na mwishowe akaamua hadi kufunga ndoa kwa hela ya DARUSO-Mimi binafsi I hate him.Ni mbinafsi saana , hao wananchi wameula wa chuya-Anpenda madaraka wakati kuongoza hawezi. Alafu Mrema john yule mkurugenzi wa CHADEMA Anamfahamu vyema maana mrema wakati huo alikuwa ni waziri mkuu wa DARUSO. Ile DARUSO bila Mrema ingekufa.Mwita hafai hafai hafai
 
Ife mara ngapi? ilishakufa limebaki jina tu! Ila kwa mwita anaendana na siasa za mara/tarime. Huko ndo kuzuri kufanya siasa zake.
 
Huyu jamaa namfaham toka UDSM. Kama mtu kaweza kujiunga na chama pinzani badala ya tawala huyo ni jasiri
 
Ndugu zangu!!

Hakuna mtu aliyekamilika, bado nashawishika kuwa pamoja na makosa yake ya nyuma, bado Mwita atakuwa ni mbunge mzuri zaidi kwa wanaTarime kuliko mgombea wa CCM.

Tumuunge mkono.
 
Mie mwenyewe namfaham fika Mwita. The guy is good. Huwezi kumlinganisha na Bahati Tweve hata kidogo. Jamaa ni mzuri na mwenye msimamo.

Huyu mshikaji alipata kura yangu pale daruso. katika uongonzi wake wa daruso namkumbuka kwa jambo moja tu. Alipoulizwa mbona tunasikia kuwa umeenda kuolea hela za daruso, alijibu hivi; kama hutaoa basi wewe utaolewa. Was funny for me. Anajazba, anamsimamo ila anafaa ukilinganisha na wengine wengi.
Thweve hamna kitu, aliishia kuuza vyumba tu alipokuwa kiongozi wa accomodation. Anatamaa na ni mjanja ila ni mwizi aka kafisadi kadogo, so akipata nafsi itakuwa balaa.
 

Hebu basi turejee kwenye mapungufu yako maana naona wewe ni kiranja wa kutaja ya wenzio.
 
Mwita Waitara Mwikwabe, huyu huyu aliyekuwa kiongozi wa DARUSO, akaamua kutusaliti, akawafuta kazi wale wote aliowahisi walikuwa wanapinga utawala wake uliokuwa umesheheni ubinafsi. Aliingia akiwa amevalia gwanda lililosadifu upiganiaji haki ulokomaa hakika hakuna aliyeweza kudhania kuwa alikuwa amevalia suti ilojaa usaliti.

Mbunge wa Sasa Charles Mwera ni kweli yuko na mapungufu yake kama mwanasiasa ila hilo halina ubishi lakini kama wanatarime wanadhani Mwita Waitara ni mkombozi aliyeshuka kwa ajili ya kuleta ukombozi wa kweli hakika wameruka majivu na kujikuta wakikanyaga moto wa gesi. Hata wana UDSM miaka kadhaa ilopita tuliamini hivyo na tulianza kulia na kusaga meno. siwashawishi waamini haya, nawashawishi wamchague ili nao wapate machungu tuliyoyapata kutokana na usaliti wake.

Huyu ni msaliti mwenye uwezo wa kujivika sura ya ukombozi ni adui wa demokrasia
 


wewe humfahamu vizuri ,namfahamu tangu anasoma azania alikuwa headboy wa pale .ni kujipendekeza kwa walimu na ubinafsi.kama unakumbuka mwaka 2004 udsm aliuza vyumba nusu ya vilivyopo,watu walitaabika sana napenda upinzani lakini kwa mwita hapana ,hapana,hapana .bora rostam kuliko mwita waulize wanafunzi waliokuwepo udsm 2004 watakwambia mwita mwikabe nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…