kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Watu wanaweza kuhamishwa na kuishi magorofani lakini wanyama, mifugo, madini na kilimo lazima viishi ardhini, Mwita hataki watu wa tarime wasogezwe kupisha mbuga ya Serengeti lakini anaona ni sawa watanzania wengine kuhamishwa Ngorongoro na wengine kuhamishwa kupisha ujenzi wa viwanja vya ndege (Kipawa), mabomba ya gesi (Mtwara), kupisha Bomba la mafuta (Tanga, Chongoleani), migodi ya madini (Shinyanga, Mwanza), ujenzi wa barabara ya njia 6 (Kimara na Ubungo), nk.
Anatumia nguvu nyingi kuzuia Serikali isiweke vigingi vya mipaka kati ya hifadhi na wananchi. Huu sio weledi. Weledi ungekuwa kipinga kila kabila na kila mwananchi anaehamishwa kupisha miradi ya maendeleo na hifadhi.
Wananchi wake wanaweza pia kuhamishwa kama wale wa Ngorongoro walivyohamishiwa Msomera, Handeni, wale wa Kipawa pale walivyopisha ujenzi wa terminal 3 pale DSM.
Hata Waziri wa Kilimo awe macho na watu wanaopima ardhi yenye rutuba kuigeuza viwanja vya nyumba kwa visingizio vya ovyo ovyo kwamba mji unapanuka, kuna wakati watu wajenge kwa kwenda juu ili watoshe wote kwenye eneo dogo na kuacha kilimo na mifugo vipate nafasi.
Anatoa machozi ya kinafiki kabisa huyu jamaa.
---
Pia soma > Mbunge Mwita Waitara amwaga machozi mbele ya Wanahabari