Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Hapa inabidi tutafakari uwezo wao wa kufikiri unatokana na shule ndogo , au njaa, hivi wanajua Mkoa wa Tabora na watu wake ni mojawapo wa jamii zilizo nyuma kimaendeleo kutokana na kuchagua viongozi wabovu,ndio maana wana madini lakini hawana kitu, barabara ndio wanapata leo hii baada ya miaka 40 ya uhuru, na kufanywa watumwa wakulima tumbaku, ambayo inakuwa processed sehemu nyingine. Infact nafikiri wananyimwa maendeleo ili waendele kuwa watumwa na wao hawalioni hilo, akija fisadi mija akawapa Vi T-shirt ndio yanakuja mambo kama haya
 
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora


Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake


Mengi, kama Mtanzania yeyote yule ana uhuru na haki ya kutoa maoni yake. Mnajua maana ya kuhukumu?





Msituhadae Watanzania. Tuna uwezo wa kuchambua pumba na mchele. Mtu yeyote atakaye tumia uhuru wake wa kutoa maoni vibaya atapelekwa mahakamani na huko sheria itachukua mkondo wake.





Rostam kuwa Kada wa CCM hakumfanyi awe mungumtu au malaika. Nae ni binadamu na anakosea. Mwananchi yoyote ana haki ya kutoa maoni yake pale anapoona mwenzake amekosea.



Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania


Hili mnalielewa vizuri au mmenukuu tu?


lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.


Msiwafanye Watanzania hawana akili.





Mengi ametumia uhuru na haki yake kutoa maoni yake. Kama kauli yake imemkwaza mtu, huyo mtu ana uhuru na haki ya kwenda mahakamani kufungua kesi. Ushahidi wote na ukweli utapatikana huko.



Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.


Hiyo ni kazi ya mahakama. Na kama kauli za Mengi ni ukweli mtupu itakuwaje? Mmelifikiria hilo?






Mlikua wapi mwaka 2005?




Hapa ni dhahiri kwamba mnaongea kwa niaba yenu wenyewe na sio Watanzania wote.



ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu.

Rais sio Mungu. Nae huwa anakosea. Kila mwananchi ana haki ya kumkosoa Rais sababu hii ni nchi yetu sote na si yake pekeyake.
 
Last edited:
Wahenga walisema, ''Is better to keep silence rather than exposing your ignorance'' Sorry that, UVCCM have dared to expose their profession omission and ignorance.
 
jamani, Mengi siyo mtu wa kwanza kuwataja mafisadi hadharani. Tena mbona Mengi ameawataja wachache! Mmeisahau ile orodha ya mafisadi iliyotajwa na akina Dr. Slaa ya watu 11??

Na wakatishia kwenda mahakamani, jambo ambalo hawakulifanya. Mie ni kijana wa CCM, nadhani hawa vijana wenzangu wamekurupuka. RA atakuwa amewashikisha mshiko tu; njaa zao!
 
jamani, Mengi siyo mtu wa kwanza kuwataja mafisadi hadharani. Tena mbona Mengi ameawataja wachache! Mmeisahau ile orodha ya mafisadi iliyotajwa na akina Dr. Slaa ya watu 11??

Na wakatishia kwenda mahakamani, jambo ambalo hawakulifanya. Mie ni kijana wa CCM, nadhani hawa vijana wenzangu wamekurupuka. RA atakuwa amewashikisha mshiko tu; njaa zao!
 
Jamani, ngoja kwanza niwaambie wadogo zangu kwa Kinyamwezi na baadaye ntakuja na nyingine nikikusanya data:-

Vazuna vane, mwavimbelwa kihembe. Vasunkuni inywe!!
 
Mengi alisema kuwa hawa wanatuhumiwa kwa ufisadi mkubwa, Manji akaona kuwa ni kashfa, hawa sasa wanataka kuligeuza hili suala kuwa la kisiasa. Haya tuendelee tuone tutasihia wapi
 
Vijana wa CCM bwana, wametuonesha wao ni watu wa aina gani. Wametoka point 11 kila moja thamani yake si chini ya $10,000. Kwa hiyo mamabo yao supa, wana zaidi ya $100,000 mfukoni!!

Ila wakumbuke Tabora ni miongoni mwa mikoa ambayo bila reli ya mjerumani hufiki! Swahiba wao RA atawanunulia helikopita mwakani!!
 
Hapo ndio wamemalizia kabisa kuwa watakufa naye.
 
hao ndo viongozi wa kesho wanaoandaliwa na chama hao. hehe
 

Kama wewe ni kijana wa CCM wewe pia ni sehemu ya tatizo na inabidi umulikwe.
 
It is so unfortunate, tunajadili watu kila siku badala ya kujadili issues, hawa "wajomba" kutoka Tabora nani kawapa nauli?
 
Wabongo wengi lini tutafungukaaaaa???

hizi kelele zinaongeza kwa kasi umaskini wetu au??

Mengi mwana CCM!!!! Maana anaonekana kukipenda sana hicho chama mpaka anakisaidia kupitia media zake kiwatose hao MAFISADI PAPA(KM MANJI NA RA) ili kiweze kushinda vizuri...

Maoni yake kuhusu JK ni kama ile ripoti ya REDET! (Ananichanganya sana)
 
Sishangai,Tanzania hata ukienda Polisi kutoa taarifa ya suala la uhalifu uliotokea eneo lako kama mauaji au uvamizi fulani unawekwa ndani wewe ili uisaidie polisi kwa upelelezi.
Hii inatokea Tanzania tu,hakuna mahali pengine utakuta mambo kama haya.
Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…