Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,768
- 2,361
jk tunakupenda , jiokoe na kundi la mafisadi kunagaubaga before it is too late!!!!!tatizo kubwa ni kuwa, joto la moto uliowashwa dhidi ya ufisadi unazidi kuwakaribia mafisadi wote. Hii ndio sababu zinatafutwa kila mbinu za kuuepushia mbali ili joto lake lisije waoka.
Bottom line ni kwamba S Simba and G Mkuchika wametoa maoni yao kama mawaziri wa ziwara zao na sio tamko la serikali..... Serikali ya Tanzania itoe tamko hafifu kama hilo?? Whom am I kidding, it is an alinacha style of Govt anyway!!!
This is the saddest thang that has happened to Tz in its more than 45 years history...... we need some help and faaaast!!!
Utarudisha chenji kijana......Yangu macho...Movie ndio kwanza inaanza... Ngoja nichukue Popcorn zangu kopo za Tusker niangalie... Mpaka 2010...Zitaibuka Movie nyingi tu...
Mi nadhani huyu sofia simba ni hawara ya rostam aziz kwa sababu kama ana akili asinge tetea wahindi wanaoiba mali ya watanzania maskini na kupeleka canada na kwingineko. Hivi huyu mama ana mume kweli??au ana mume *****?? si ajabu rostam ndo ngoma yake!!!
Ah.... mpaka inachefua. Hivi rais alitoa wapi viwaziri pambafu kama hivi???
Morani, mmoja ni Waziri wa Utawala Bora na mwingine wa Habari, Utamaduni na Michezo. Wizara zao zinahusika moja kwa moja na Mengi na kile alichokisema. Na walipozungumza walizungumza kama Mawaziri wa serikali na hivyo kusema kwa jina la serikali. Kimsingi tunaweza kusema "Serikali yasema Mengi Kachemsha"!
Sasa hao ndio mawaziri wetu a.k.a ndiyo serikali yetu.
Mawaziri ni mawaziri katika serikali gani? Na kama wametoa tamko official linakuwa tamko la nani?
Bado mwawashangaa mawaziri wa jk? ......
Na Manyerere kaandika hivi:
Reginald Mengi ni msafi kiasi gani?
Na Manyerere Jackton
NILIANZA kumjua Reginald Mengi, mwanzoni mwa miaka ya 1990. Siku moja, tukiwa nyumbani Msasani, alifika getini. Akazungumza na walinzi. Akaangaza huku na kule kutazama mandhari ya mahali hapo ambako ni nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
lakini huyu anasema mengi alikwenda nyumbani(kwao) msasani kwa mwalimu.....nauliza tu kama nae ni mmoja wa wanafamilia ya mwalimu....Duniani wawili wawili nikama FMES alivyofanana na JW Malecela, ama Dilunga na Kuhani ila wote hawa hawajuani kabisa.......unaweza kuta Masanilo ni Yo Yo
Wahariri: Manyerere Jackton & the Gang
Acid|Burn20th June 2007, 04:53 PM
Katika issue ya gazeti la Mwanahalisi la week iliyopita (ambayo sikuisona) walireport wahariri wa magazeti wanaotumia majina bandia kwajili ya uchafuzi na kuwa vibaraka wa serikali.
Majina ya hao wahariri bandia ilikuwa ni Joseph Ryasembe na Mwakyembe Mwakyanjala.
Sasa katika issue ya week hii, nilifanikiwa kusoma, kuna makala moja ya mwandishi anasifia gazeti kwa kutoa majina halali ya hao waandishi bandia Ryasembe na Mwakyembe.
Anaelezea jinsi Maggid Mjengwa alivyowahi kuhoji Ryasembe anavyoandika makala kama "Proffesional journalist" lakini haonekani kamwe wakati wa amani bali wakati wa shari, ushindani na mvutano wa kuvuana nguo.
Huyu mwandishi ndio aliyeandika makala ya matusi dhidi ya Dr. Salim wakati wa kinyangajiro cha kuafuta mbombea wa urais wa CCM.
Alimtuhumu Dr. Salim ya kuwa hafai kuwa rais kwasababu "ni mwarabu," na kwamba nchi hii haiwezi kutawaliwa na mwarabu, na kwamba ingawa Mwalimu Julius nyerere alimpenda sana. Na pia WTZ wasingemkubali awe rais kwasababu aliwahi kuwa mwanachama wa Hizbu, Zanzibar.
Yalizushwa mengi dhidi ya Dr. Salim kwamba ndugu zake wapo Uarabuni wakiwa wameshikilia nafasi za juu katika jeshi la nchi hiyo na kwamba kwa yeye kupewa nafasi ya juu ya urais kutaiweka nchi katika mazingira magumu.
Ikumbukwe kwamba, ni katika kipindi hicho uhuma kwamba dr. salim alihusika na mauwaji ya Rais wa kwamba wa Zanzibar, Karume zilibuliwa.
Hadi sasa hakuna Kiongozi yeyote wa serikali au hata chama tawala, aliyejitokeza kumtetea Dr. Salim.
Ni Ryasembe pia aliyewashambulia kina Jenerali Ulimwengu na Spika Mstafu Pius msekwa kwa maneno na kejeli ambazo siwezi hata kuziandika hapa lakini alikuwa akimkemea ulimwengu kwa kuonekana anampenda na kumwamini Dr. Salim na alishambulia Msekwa kwa kugombea uspika dhidi ya Samuel Sitta aliyekuwa akionekana kipenzi cha wale waliojulikana kama wanamtandao.
Ni jambo la aibu kuona baadhi ya wahariri wakiambatana na wanasiasa na kuchafua majina ya wenzao au wapinzani na maswahiba wao kwa madhumuni ya ujipendekeza kwa wakubwa.
Lakini jambo kubwa hapa kwa mujibu wa habari za gazeti hili ya MwanaHalisi, ni jinsi gani mhariri wa RAI, Muhingo Rweyemamu, anastahili pongezi kwa kukataa kuchapisha makala ya uchaguzi iliyotumwa kwake na huyo mwingine anayejiita Mwakyembe Mwakyanjala, yenye kulenga kuchafua jina la gazeti jingine na mhariri wake, wakidai wametumwa na mtu kiongozi mojja waliyemwita "Mr. Mvi"
Mwandishi huyu Ryasembe imegundulika ni Manyerere Jackton mhariri wa Tanzania Daima
NB: kwenye makala hiyo niliyosoma sikubahatika kuona jina la Mwakyembe Mwakyanjala. ila jina lake lipo katika Issue ya gazeti lililopita, Naomba Maggid Mjengwa utupe jibu, kwa namna moja au nyingine utakuwa ulilisoma kwasababu nimeona makala yako ya michezo katika toleo la week hii.
Mwenye kujua "Mr. Mvi" ni nani atueleze.
hivi ni manyerere huyu huyu mchonganishi, mpenda rushwa, mwenye chuki aliyeandika hii ama ?Na Manyerere kaandika hivi:
Reginald Mengi ni msafi kiasi gani?
Na Manyerere Jackton
NILIANZA kumjua Reginald Mengi, mwanzoni mwa miaka ya 1990. Siku moja, tukiwa nyumbani Msasani, alifika getini. Akazungumza na walinzi. Akaangaza huku na kule kutazama mandhari ya mahali hapo ambako ni nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ili kuona vizuri, alizunguka hadi nyuma ya kibanda cha walinzi. Akarejea mbele ofisini. Akatikisa kichwa. Kwa sauti yake ya upole, akasema, Baba wa Taifa hawezi kuishi katika mazingira kama haya. Naomba mfikishie ombi langu kwake. Nataka nimjengee fensi. Hii sengenge haifai.
Wale maofisa Usalama wa Taifa waliokuwapo, waliheshimu kauli hiyo. Wakati huo Mwalimu alikuwa Butiama. Baada ya siku chache, Mwalimu aliwasili Msasani. Mmoja wa viongozi wa Usalama akabeba msalaba wa kumweleza Mwalimu ofa aliyopewa na Mengi.
Mwalimu akabadilika. Uso ukawa mwekundu. Akatafuna midomo kama ilivyokuwa ada kwake baada ya kuguswa na jambo zito. Mwalimu akahoji, Mengi nani? Katoa wapi utajiri wa kunijengea fensi? Huyu ni (akatukana). Kama ana hela akawajengee masikini; wapo wengi wanaohitaji msaada. Sitaki kusikia upumbavu wa kunijengea fensi, kwani ameona hii fensi (ya nyaya, tena zilizochakaa) hainitoshi? Mwambieni sitaki kabisa.
Kweli, Mengi hakuonekana tena kwa Mwalimu, labda wakati wa msiba. Tangu siku hiyo, nikawa nataka kujua sababu za mtu huyu kuchukiwa na Mwalimu. Mwalimu alikuwa kiona mbali. Pengine alijua kwamba akiruhusu Mengi amjengee hiyo fensi, baadaye yangekuwa matangazo kuanzia kwenye televisheni, redio hadi magazeti anayoanzisha kama uyoga.
Mwalimu alipofoka kuhusu msaada wa Mengi, alifoka kwa sababu alijua Mengi si msafi kama anavyotaka jamii imtambue. Alijua Mengi jinsi alivyofaidi fedha kutoka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mali ya wananchi, lakini akawa anakwepa kulipa kwa kutumia wanasheria. Hadi leo bado Mengi anakabiliwa na utata mkubwa kuhusu mabilioni aliyokopa yeye au familia yake.
Mwaka 1996 aligombana na viongozi wa Habari Corporation Limited, iliyokuwa ikiongozwa na magwiji wa habari, kina Jenerali Ulimwengu, Johnson Mbwambo, Salva Rweyemamu, Dk. Gideon Shoo na wengine. Chanzo cha ugomvi kilitokana na kuandikwa kwamba anadaiwa mamilioni ya NBC.
Juzi, Mengi ameibuka kwenye vyombo vya habari. Akawa mlalamikaji. Akawa mwendesha mashitaka. Akawa jaji. Akatoa hukumu. Alifanya kile alichofanya kwa kigezo kwamba anapambana na mafisadi. Hivi kina Edward Sokoine, ambao ndiyo wanaoheshimika katika vita hiyo, wangetumia staili hii, nchi ingekuwaje? Mengi ni nani wa kuwahukumu wengine?
Kama ilivyotarajiwa, baada ya kubwabwaja, akawageukia wananchi. Akataka wamuunge mkono. Tena akasema anajua maisha yake yake yako hatarini! Hizi ni propaganda tu. Nani ambaye maisha yake hayako hatarini, hasa wakati huu ambao hata bajaj zinaua?
Akianzisha ugomvi, anataka wananchi wote wamuunge mkono. Wampigie makofi. Akilia, tulie naye. Akicheka, tucheke sote. Mengi anaweza kuanzisha ugomvi kisha akawataka Watanzania wote wamtetee. Akikosa biashara, basi huyo aliyemshinda kwenye biashara hiyo, ni fisadi. Atahamishia ugomvi kwenye televisheni yake.
Amegombana na kila kundi katika jamii. Amegombana kuanzia kwa maaskofu hadi kwenye kundi la Ze Comedy. Fikiria. Kama mtu anaweza kugombana hata na viongozi wa kiroho, huyo lazima atakuwa na matatizo.
Yeyote anayemwangalia vema Mengi kwenye televisheni, atagundua kuwa huyu Mtanzania mwenzetu anaelekea kuchanganyikiwa. Inawezekana kabisa akili ya leo ya Mengi si akili ile aliyokuwa nayo alipoanza harakati za kujikomboa kiuchumi. Amejisahau mno kwa kudhani kwamba wananchi wote ni wajinga.
Mengi wa leo amekuwa wa kukomoa wenzake kwa kivuli cha kupambana na mafisadi. Yeye ana usafi gani? Hivi kweli katika kundi la watoa rushwa, Mengi ataponea tundu gani? Juzi alipotaja hao anaowaita mapapa wa ufisadi, aligawa shilingi ngapi kwa kila mwanahabari? Mimi najua alitoa kiasi gani. Aseme usafi wake uko wapi?
Hakuna Mtanzania mwenye akili timamu anayeweza kujiweka nyuma katika mapambano dhidi ya ufisadi. Mara zote tumekemea na hata kuibua ufisadi katika wizara, idara na kila mahali katika jamii yetu. Ushahidi wa ushindi tulioupata upo.
Lakini vita dhidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi yetu tumeiendesha kwa misingi ya haki na kwa utu. Wapiganaji wa kweli hawawezi kutumia nafasi ya vyombo vyao vya habari, kuwadhalilisha watu wengine.
Mengi anawatukana wenzake kwa sababu anajua kwamba ana vyombo vya habari vinavyotazamwa, kusikilizwa na kusomwa na wananchi wengi-ndani na nje ya nchi. Anajua masikini hawa wenye rangi nyeupe wataonekana wa ajabu wakianzisha televisheni maalumu ya kumshughulikia Mengi.
Kama tunaweza kulaani matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi na watumishi wa Serikali, kwa nini Mengi asilaaniwe kwa matumizi mabaya ya vyombo vyake vya habari?
Hivi, tajiri Teddy Tunner, ambaye ni mmiliki wa kituo cha televisheni cha CNN, akiamua kufanya kama haya yanayofanywa na Mengi, mambo yatakuwaje? Lakini tofauti na Ulaya na Marekani, hapa Tanzania kuna kina Mengi wanaosimama na kutukana wengine, kisha wakaachwa hivi hivi. Sana sana mtukanaji eti anamweleza anayetukanwa, ukitaka nenda mahakamani.
Mengi amefika mahali amejisahau. Ameona anaweza kutumia silaha yoyote kufanikisha malengo yake anayoyajua yeye mwenyewe. Mengi anajua kwamba nchi yetu inafuata misingi ya kisheria. Tuna Mahakama, Bunge na Serikali. Kila chombo kinawajibu wake. Tuna Takukuru na vyombo vingine vingi tu. Kama ushahidi anao, kashindwa nini kuupeleka katika vyombo hivyo? Kama ameupeleka, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa, wa kulaumiwa ni mtuhumiwa au anayestahili kuwashitaki? Kwa nini mtuhumiwa atukanwe na kudhalilishwa?
Anajua fika kwamba baadhi ya watu anaowashambulia hadharani wana kesi mahakamani. Anajua kuwa Mahakama inapokuwa kwenye shughuli zake, inapaswa iheshimiwe. Ipewe wigo wa kupitia mashitaka na utetezi ili ifikie hatua ya kutoa hukumu ya haki. Je, katika mazingira ya aina hii, mazingira ya kutukanana, kubezana, kusemana ovyo, mahakama itakuwa na kazi gani?
Kama kweli Mengi alikusudia kuwataja mapapa wa rushwa, basi angewataja hata wale wenye rangi nyeusi! Kama hawa weupe wamechukua fedha, nani kawapa huko BoT. Je, BoT kuna gavana Mhindi au Mzungu? Yeye alipochukua fedha NBC, kulikuwa na mkurugenzi Mhindi au Mzungu? Je, mawaziri wanaoidhinisha, ni wa kutoka nchi gani? Hawa kwa nini asiwaunganishe? Kwa nini achague hawa wenye rangi tofauti tu?
Angewataja na kina Manyerere wenye ngozi nyeusi ili walau watu wajue kwamba anachofanya anakifanya kwa misingi ya haki. Lakini kutamka wazi kwamba hawa wenye asili ya Kiasia ndiyo watu hatari, ndiyo wanaoimaliza nchi, ni kutafuta tu kuungwa mkono na jamii ya watu masikini. Kuna Wahindi na wazungu waliofanya mambo mengi mazuri katika nchi hii. Kina Dereck Brycson, Alnoor Kassum, Amir Habib Jamal, Shamim Khan, Joan Wicken na wengine wengi.
Mengi amekuwa makini sana kutafuta sympathy kutoka jamii. Mara zote anatafuta mambo ambayo anajua akiyateremsha kwenye jamii, ataungwa mkono. Akishawaandalia chakula walemavu na watu wengine masikini, hazitopita siku nyingi, ataibua bomu.
Haya tumeyaona mwaka 1994 aliponunua ugomvi kwa nguvu kutoka kwa Watanzania wenye asili ya Kiasia, hata akafika hatua akadai kwamba kulikuwa na mpango wa kumtoa roho.
Rais wa wakati huo, Mzee Ali Hassan Mwinyi, akapata habari hizo. Mengi akapewa ulinzi wa askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU). Tena wengine walikuwa wakilinda kwa Mwalimu Nyerere. Wakatolewa ili wamlinde Mengi. Hakuna aliyelalamika maana Katiba ya nchi inazungumzia haki ya kila mwananchi kupewa ulinzi na hifadhi ya maisha yake.
Baadaye ikaja kubainika kuwa ugomvi ule ulitengenezwa na Mengi mwenyewe, akitaka wananchi wamwonee huruma. Hata alipokuwa akiuhadaa umma wa Watanzania kwamba matangazo ya mpira au ngumi yalikuwa yakiletwa moja kwa moja kutoka Ulaya na Marekani, akasema anasakamwa na wabaya wake. Ukweli ulikuwa kwamba badala ya matangazo yale kuwa yanatoka moja kwa moja Ulaya, yalikuwa yanatoka moja kwa moja Mikocheni!
Mengi, kama nilivyosema hapo awali, aligombana na maaskofu na wapinga matumizi ya kondomu. Yeye anajua wazi kwamba makanisa yana miiko. Hayaongozwi na utashi wa wamiliki au wenye hisa kwenye viwanda na biashara za kondomu. Akatetea kondomu hadi akaitwa nabii wa kondomu.
Bwana mkubwa huyu huyu aligombana na Wilson Masilingi baada ya kunyimwa umiliki wa hoteli ya Kilimanjaro. Hatuna hakika kama hoteli hiyo angepewa Mengi, ingekuwa na mwonekano mzuri na wa maana kama huu uliowekwa na mwekezaji aliyepewa.
Alishagombana na Shamin Khan, wakati huo akiwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara. Mengi akawa anawanywesha watu maji ya kisima, lakini akitangaza kuwa ni ya chemchem kutoka mlimani. Waligombana wee, hadi Khan akaibuka mshindi. Maneno ya udanganyifu yakafutwa kwenye chupa za maji. Udanganyifu nao ni ufisadi.
Huyu huyu Mengi amegombana na Yusuf Manji. Amemtukana kadri alivyoweza. Akawaingiza hata baadhi ya wanasiasa mamluki ili wamtukane. Hapa naomba wasomaji watambue kuwa simtetei Manji au hao aliowabatiza kuwa ni mapapa wa ufisadi. Ninachotetea hapa ni maadili na namna ya kuwasilisha jambo. Kumparamia mtu na kuanza kumtukana kwa sababu tu mmenyanganyana michezo ya bahati na nasibu na kamari, si jambo la kiungwana.
Wiki kadhaa zilizopita alimvaa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha. Kila aliyefuatilia ugomvi ule kwa makini, alimshangaa Mengi. Mtu mzima kubishana, kutukanana na mtu mwenye hadhi ya mwanao, ni aibu.
Kutoka kwa Masha ameingia kwa wahariri kadhaa wa vyombo vya habari. Yeye kila siku anasimama kudai kwamba mafisadi wanaanzisha magazeti kumshambulia. Lakini anapuuza upande wake. Yeye kila anapokabiliana na mtu au kikundi cha watu, si ajabu tukaona gazeti maalumu kwa ajili ya kukabiliana na mtu au kundi alilokorofishana nalo.
Ni wapi ambako yeye anapata fedha safi za kuanzisha magazeti ambako wengine hawawezi kuzipata? Kuna vijana wamejiunga. Wameanzisha magazeti kwa nia njema, lakini ameingilia kati na kusema wamefadhiliwa na mafisadi.
Makala hii itazua mjadala. Nitafurahi sana mjadala huu ukiendelea. Mengi ameshapeleka uwongo hadi Ikulu akiwasingizia waandishi wa habari kwamba wameunda umoja kumchafua Rais Kikwete. Sina hakika, lakini inawezekana ndiyo mbinu yake ya kujipendekeza ili awe karibu na Rais Kikwete. Anajua hakumuunga mkono Kikwete wakati wa mchakato, sasa kufukia hayo, anafanya kila awezalo ili awe karibu naye. Lakini wenye akili wanajua hakuna kiongozi makini anaweza kufunga pingu za urafiki na Mengi. Hana uadilifu huo.
Ataibuka na kusema nimetumwa na mafisadi. Atasema nimelipwa ili nimwandike. Bora aseme uwongo huo, lakini nimeshindwa kuvumilia usanii huu anaoufanya sasa. Tumefanya kazi Habari Corporation kwa miaka mingi kabla ya kampuni hii kupata wamiliki wengine. Leo hatuwezi kukosa amani kwa sababu Mengi anatusema kwamba tumeajiriwa na mafisadi. Yeye ameuza kampuni ngapi? Siwezi kuendelea kukaa kimya na kumpa heshima haramu.
Mengi hana usafi huu ambao anataka watu waamini kuwa anao. Hana. Anapoamua kuwatukana wengine, lazima ajiridhishe kwanza kwamba yeye ni msafi. Hata Biblia inasema usikazane kukinyooshea kidole kibanzi kilicho kwenye jicho la mwenzio wakati lako lina boriti!
Lakini hatari kubwa ni hii ya kuanza kuhubiri maneno yanayoweza kuibua chuki kubwa miongoni mwa wananchi. Hakika, kwa maneno ya kusema Wahindi ndiyo waporaji wakuu wa uchumi wa nchi hii, anataka kuwaeleza wananchi kwamba sasa waanze kuwachukia. Kwa nini udhaifu wa Waafrika kuongoza nchi na kumiliki uchumi wanasukumiwa Wahindi na Wazungu? Tangu Uhuru mwaka 1961, tumekuwa na rais yeyote Mhindi au Mzungu? Udhaifu ni wetu wenyewe.
Kwa maneno yake, sijui itakuwaje Watanzania wenye asili ya Kiasia wakiharibikiwa gari Manzese au Mwanjelwa. Je, hawatashambuliwa? Je, wakishambuliwa, kitu gani kitazima mwendelezo huo? Mengi anaipeleka wapi Tanzania? Yeye amezeeka. Amekula chumvi ya kutosha. Awaache vijana wadogo nao wawe wazee kama yeye.
Mengi ni mtuhumiwa wa ufisadi kama watuhumiwa wengine. Bahati yake ni kwamba hakuchota fedha za EPA. Tofauti na hapo, ni fisadi tu hata kama si wa fedha, basi wa tabia.
Wakati sasa dunia ikiwa kwenye mtikisiko wa uchumi, Mengi yeye yuko kwenye mtikisiko wa akili. Amekosa busara! Angekuwa na busara, vita dhidi ya mafisadi angeishiriki kiungwana kama wanavyofanya wenzake.
Kama nilivyosema, huu ndiyo mwanzo wa mjadala. Kama yeye amekuwa mbele kuwasema wenzake, naye avumilie kusemwa. Kama kutukana watu wengine ni ushujaa, ipo siku naye atakutana na vichaa watakaomtukana.
Kuendelea kumnyamazia Mengi ni kuitoa rehani amani ya nchi yetu. Kumwogopa hakuwezi kusaidia kumrejesha kwenye mstari. Leo anatangaza hatari kama hii kupitia vyombo vyake vya habari, kesho kitu gani kitamzuia iwapo ataamua kutumia vyombo hivyo hivyo kutaka rais angolewe? Huyu ni hatari kama zilivyo hatari nyingine zinazoikabili nchi yetu. Wazanaki wanasema, nyambisabisa obhurweri, ekiriro kirambura. Tafsiri nitaitoa toleo lijalo.
manyerere@hotmail.com
0713 335469