BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Zoezi la uandikishaji Wananchi kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) limefanyika katika Kata ya Goweko huku kukiwa na mwitikio mkubwa unaoonekana kuzidi idadi ya Watendaji na vifaa vinavyotumika.
Idadi ya Wananchi waliojitokeza ni takribani 500 ambapo kuna Watu wengi wanaotakiwa kulipia Tsh 200 hadi 400 ili kupata nakala ya fomu ya kujaza.
Idadi ni kubwa na huduma ni hafifu, ninachojiuliza ni kosa Kisheria kutumia laini iliyosajiliwa kwa Namba ya NIDA ya mtu mwingine, ninachojiuliza kama hao wote hawatakamilisha mchakato na wanahitaji laini za simu maana yake watatumia NIDA za watu wengine?
~ Waliofanya Uandikishaji Vitambulivyo vya NIDA, Nsololo - Uyui hawajakamilisha kazi, bado watu wengi hawajakamilisha mchakato
~ NIDA yatoa majibu ya changamoto zinazolalamikiwa katika Uandikishaji Vitambulisho vya NIDA Wilayani Uyui Mkoani Tabora