Madibira 1
JF-Expert Member
- Jan 6, 2023
- 358
- 831
Jamaa mmoja anaejulikana Kwa jina la David (27) mkazi wa Madibira ,mbarali mkoani mbeya ameoa mke wa mgoni wake. Bwana David alimuoa Maria (23) mwaka 2019 nabkibahatika kupata mtoto mmoja. Kutokana na changamoto za kiuchumi alizokua akipitia kijana huyo ilipelekea mke kumkimbia jamaa mwaka jana na kwenda kuolewa kama mke wa pili Kwa bwana Kelvin (36).
Bwana Kelvin alimuoa bi. Frola (,32) mwaka 2017 ambae wakati anamuoa na kufunga nae ndoa alikua na mtoto wa mwaka mmoja na nusu(, mtoto wa kufikia,) kutokana na kuishi kwa miaka 6 bila kupata mtoto Kwa mwanamke huyo wa ndoa bwana Kelvin aliamua kutafuta mwingine. Katika kutafuta mwingine ndio akampata aliekuwa mke wa David na kumuoa.
Ikumbukwe kuwa David na Maria hawakufunga ndoa ila walikua wakiishi Kama mke na mume kwa miaka minne. Hivyo kitendo cha kelvin kumuoa Binti huyo David hakukubaliana nacho ikizingatiwa bado anampenda mkewe lakini ugumu wa maisha ndio uliomkimbiza. Hivyo bwana David aliapa kulipa kisasi.
Mwaka huu kabla ya ijumaa kuu bwana David aliweka mke ndani. Jambo ambalo haikutarajiwa na wengi ni kuwa mke aliewekwa ndani no yule mke mkubwa wa bwana Kelvin. Kwahiyo bwana David ni kama amelipa kisasi Kwa bwana Kelvin Kwa kubadilishana wake.
Changamoto ni kuwa wote wanaishi mtaa mmoja. Bwana Kelvin akamvamia kijana na kumpiga kisa kaoa mke wake jambo lilipelekea kuwepo na kikao Cha kifamilia hapo Jana.
Kwenye kikao ilibainika kuwa bwana Kelvin anampenda mke mkubwa ingawa alimtelekeza lakini bado anampenda. Mariam anampenda David lakini Hana namna lazima atumikie ndoa mpya. Bi frola hampendi Tena kelvin upendo upo Kwa David.
Maoni ya wengi yanonesha David kapoteza kwasababu ameachana na Binti maria Mika 23 na kumuoa bi Flora Miaka 32. Lakini tujadili kidogo. Maamuzi ya vijana hao nani kazingua? Karibuni.