Mwizi anaruhusiwa kuwekeza kwa pesa ya wizi?

Mwizi anaruhusiwa kuwekeza kwa pesa ya wizi?

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2019
Posts
370
Reaction score
1,189
Nisaidieni utata huu. Je, ni sahihi pia kama mwizi akiiba halafu fedha ile akaiwekeza?

IMG_3513.jpg


===
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Kenya, Nancy Gathungu amependekeza watu wanaoiba fedha za umma wawekeze nchini humo ili kuchochea maendeleo, badala ya kuzificha nje ya nchi. Benki ya Dunia inakadiria kuwa TZS trilioni 6 huibwa kila mwaka na kupelekwa nje ya nchi.
 
Kuna awamu inayofanana na hii fedha za wizi zilikua katika mfumo halali wa maisha.

Waliokua wanaziingiza ndio walikua wanatoa ajira na kulipa kodi.

Hivyo ni jambo ambalo liliwahi kufanyika wala sio jipya.
 
Hii kitu ni kama inaruhusiwa kwenye nchi yetu, matatizo la ukosefu wa ajira na umasikini yanatumiwa kama kichaka na wajanja kuiba pesa kisha wawekeze na kutoa ajira kwa watanzania, wanahalalisha wizi wao kupitia "wanyonge".
 
Hii ni Kenya ambapo kwa sera hii pesa yao haianguki dhidi ya US dollars
 
Unakijua kitu kinaitwa utakatishaji pesa.
Waje wakufirisi vizuri,pesa isiyojulikana umepata wapi ndiyo yale yale wanataifisha.
Wajanja sana bado wanatuona maboya
 
Inaweza kuwa mbinu nzuri kabisa ya serikali kuzipata pesa zilizoibwa😂😂
 
Back
Top Bottom