Mwizi avamia kwa ajuza wa miaka 82, bila kutarajia ajuza amshushia kipigo kizito, polisi wamuokoa

Mwizi avamia kwa ajuza wa miaka 82, bila kutarajia ajuza amshushia kipigo kizito, polisi wamuokoa

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Duniani kuna mambo. Rochester, New York Marekani, mwizi amevamia nyumba ya ajuza wa miaka 82 ambae alikua akiishi peke yake ili aibe ila mwizi alichokutana nacho hakukitegemea, ajuza amshushia kibano kizito, polisi wamemuokoa.

Huyo mwizi alienda kwa gia ya kuomba msaada kua ana tatizo ajuza amuitie gari la wagonjwa, ajuza akapiga simu kuita gari huku bado hajafungua mlango, jamaa kuona ajuza hafungui mlango akauvunja na kuingia ndani ili aibe.

Baada ya kuingia ndani ajuza wa miaka 82 ambae ni baunsa(mnyanyua vyuma) wa zamani akamkabili kwa kibano kizito, polisi wamefika na kumkuta jamaa ana hali mbaya, ajuza anasema polisi wamemuokoa, angemuua.

Waswahili husema mazarau mwiba mguu huota tende, jamaa alimchukulia poa ajuza.

1574660295794.png

 
Hahahaaaa Daaa kwamimi hata angekuwa ananyanyua treni Ajuza wa miaka 82 anishushie kichapo??
Hahhhaaaaa, mkuu hata jamaa alizarau hivyo hivyo ila alichokutana nacho ni tofauti, polisi wamefika kumuokoa jamaa na sio ajuza.

Ajuza anasema the young man picked the wrong house,, anasisitiza zaidi kua i am alone, old but guess what, i am tough.

Nimeangalia cnn nimecheka sana.
 
Ajuza alishajiandaa kisaikolojia kujihami, ila amini usiamini wapo mabibi na mababu wanamichezo/wafany mazoezi toka ujana wanapga hatarii, dunia ina mambo n muhmu tu kutumia ulimi vizuri
 
Hiyo itakuwa ni kabali,maana najaribu kufikiria huo msuli hapo kwenye mkono ndio umekamata kwenye koo la hewa,lazima pumzi zilizojirundika tumboni zitoke...
Bibi aliluka nae kavu kavu man against man sio kabali lakini jamaa kapotea kwa KO
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] heading tu ya hiyo taarifa nimecheka mpaka nimepaliwa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119]
 
Back
Top Bottom