Mwizi wa ukurasa wangu wa istagram amenirudisha sana nyuma- Ray C

Mwizi wa ukurasa wangu wa istagram amenirudisha sana nyuma- Ray C

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Rehema Chalamila 'Ray C' amedai kumfunga mwizi aliyedukua (hack) ukurasa wake wa Instagram uliokuwa na wafuasi zaidi ya laki tano na kusema kwamba hataweza kuvumilia wezi kuendelea kuwepo mitaani.

Ray C amefunguka hayo siku chache zilizopita alipokuwepo kwenye Heshima ya Bongo fleva kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa kupitia East Africa radio huku akiesema, wezi hao wa mtandaoni wanarudisha wasanii nyuma katika kufanya shughuli zao.

"Mwizi aliyedukua (hack) akaunti yangu amenirudisha sana nyuma kwani nimeshindwa kufanya matangazo ya video ya wimbo wangu, matokeo yake nimetumia nguvu kubwa sana nilipouachia. Nikimkamata huyo mtu aliyenifanyia hivyo cha kwanza nitamnasa kofi kwa kunipa kazi cha pili lazima nimfikishe polisi na mwisho wake ni Segerea. Siwezi kuendelea kuvumilia watuibie halafu waendelee kukaa mitaani kwani watatutesa sana," Ray C.

Pamoja na hayo Ray C ameongeza kwamba "Mimi akaunti yangu haijapotea kabisa kwani naiona ikiweka matangazo mbalimbali yaani nikimkamata sitamwambia anipe asilimia kumi bali atatoa pesa yote kwani nitahesababu tangazo la kwanza mpaka la mwisho ili kujua ni kiasi gani cha pesa anatakiwa anipe maana wameshazoea," aliongeza


Chanzo: EATV
 
Hiyo account ila hela? wasanii wameona instagram ndio inalipa?

sent from Sanduku la Posta using JamiiForums mobile app
 
Niseme tu wazi kuwa huyu n wakurudisha rehab
 
Mimi naona aliyemrudisha nyuma zaidi ni yule aliyemuibia akili zake na kumuingiza kwenye madawa ya kulevya na kupoteza mengi kwenye maisha yake......
 
Hana kipaji huyo,,tangu awe mteja hana tena kipaji,,wasanii wa bongo bhana.mbona zamani hakukuwa na insta wala fb wala watsap ila nyimbo zote kali ziliwika?

Mkuu tema mate chini; yumkini wewe ni mzazi pia. La muhimu ni kumuombea tu.
 
Back
Top Bottom