Mwl. Agricola-Kahororo Sekondari

PrN-kazi

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Posts
2,900
Reaction score
444
kwa wote waliosoma Kahororo Sekondari nadhani mtakua mnamkumbuka Mwl. Agricola-mtaalamu wa somo la Phyiscs, ni kwamba mwalimu wetu huyo anaumwa na yuko hapa Dar es salaam akipatiwa matibabu.

Kwa kifupi nimesikitishwa na afya ya mwalimu kuzolota: na ni vizuri kwa yeyote anayemfahamu especially wale tuliopitia pale Kahororo Sec na tuko hapa Dar tujitokeze tumpe kampani mwalimu wetu kwani anahitaji msaada wa hali na mali.

Kwasasa anapatikana Mikocheni B ila kila siku asubuhi anakuwa Ocean-road Hospital kwa ajili ya matibabu, mwenye kuitaji namba yake ya simu ni PM nikutumie.
 
PrN-kazi,
Asante kwa kusambaza taarifa. Wakati tukimwombea kwa sala, tutajitahidi pia kuendelea kujitolea kwa hali na mali kama sehemu ya kuuenzi msaada wake wa malezi na taaluma. Mungu amponye.
 
Jamani namkumbuka Mwalimu Agricola hata kama sikusoma Physics. Si yule alikuwa anaongea kwa kigugumizi hivi. Alikuwa na jina la utani nimesahau vile... (Siyo Sodium) au Archimedes?! Mpeni pole, niko nje ya Dar ningeweza kuja.
 
PrN-kazi,
Asante kwa kusambaza taarifa. Wakati tukimwombea kwa sala, tutajitahidi pia kuendelea kujitolea kwa hali na mali kama sehemu ya kuuenzi msaada wake wa malezi na taaluma. Mungu amponye.

ni kweli kiongozi; sala na kujitolea kwa hali na mali kwa mwalimu wetu ndo cha msingi haswaaa.
 
Jamani namkumbuka Mwalimu Agricola hata kama sikusoma Physics. Si yule alikuwa anaongea kwa kigugumizi hivi. Alikuwa na jina la utani nimesahau vile... (Siyo Sodium) au Archimedes?! Mpeni pole, niko nje ya Dar ningeweza kuja.

inawezekana akawa ndo huyo; ni mwalimu ambaye enzi hizo pale Kahororo alikua hana masihala na vijana wanaopenda mambo ya kiuni na kusahau kusoma.
 
.....hali ya Mwl.Agricola bado si nzuri, kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…