MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE, UNAMJUA VIZURI LAKINI?

MWL.JULIUS KAMBARAGE NYERERE, UNAMJUA VIZURI LAKINI?

Jojo123

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
432
Reaction score
703
1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe kama ya Leo 14/10/1999 kule London.Ni Raisi wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.

2.Alianza shule akiwa na miaka 12, na darasani alikuwa na akili sana hivyo akarushwa baadhi ya madarasa. Akiwa Tabora School, alikuwa ni mtoto mkaidi sana. Adui zake wakuu walikuwa ni ma-viranja (prefects). Alishitakiwa mara kadhaa kwa mwalimu mkuu na ukafikia wakati Mwalimu Mkuu akaamua Julius afukuzwe shule, mwalimu wake wa darasa licha ya utundu wake, alimpenda sana kwa sababu alikuwa na akili sana. Hivyo akamnusuru kufukuzwa shule kwa kumfanya na yeye awe kiranja (prefect).

3.Ni Raisi wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi.

4.Ni kati ya Raisi aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pengine kati ya raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.

5. Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Uingereza na Muafrika wa pili kupata Degree nje ya Afrika, akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.

6. Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hotuba yake maarufu akisema
kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana,
kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".

7. Ndio mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini- Anti Apartheid Movement mwaka 1959 pamoja na Trevor Huddleston nchini Uingereza.

8. Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.

9. Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yoyote katika historia ya ukoloni, nchi hizo ni Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975 (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990
(Namibia) na 1994 (South Africa).

10. Mwaka 2009 alitajwa na raisi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kama "World Hero of Social Justice".

11. Amepokea shahada mbalimbali kutoka, University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa),Sokoine University of Agriculture (Tanzania), and Lincoln University (PA, USA).

12. Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba 1975, Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico 1975, Order of Amílcar Cabral Guinea Bissau 1976, the Nehru Award for International Understanding in 1976, the Third World Prize in 1982, Order of Eduardo Mondlane
Mozambique 1983, the Nansen Medal for outstanding services to Refugees in 1983, Order of Agostinho Neto Angola 1985, Sir Seretse Khama SADC Medal 1986, Joliot-Curie Medal of Peace 1988, the Lenin Peace Prize in 1987, the International Simón Bolívar Prize in
1992, and the Gandhi Peace Prize in 1995, Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi 2000, Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold) South Africa 2004, Royal Order of Munhumutapa Zimbabwe 2005, Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master) Uganda 2005, Order of Katonga Uganda 2005, National Liberation Medal Rwanda 2009, National Liberation Medal Rwanda 2009, Campaign Against Genocide Medal Rwanda 2009, Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis Namibia 2010, Tanzania Professional Network Award 2011, Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Tanzania 2011, National Order of the Republic (Grand Cordon) Burundi 2012 and Order of Jamaica, Jamaica.

13. Mwaka 2007 Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo, Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.

14. Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km)
and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region, Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.

15. Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha
Declaration, Education for self-reliance, The varied paths to socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, na Uongozi na Hatima ya Tanzania.

16. Pamoja na kujulikana kama - Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.

17. Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha - pia alikuwa akifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.

18. Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopia kama mtu pekee duniani katika historia ya karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.
 
Championed the release of Jomo Kenyatta from detention in Kenya
 
Huwa najiuliza kama kuna kiongoz wa africa aliyekuwa na sifa hata nusu za huyu mtu... Nashangaa hata Mandela alivuma kwa lipi hasa.. Maana hata robo ya sifa na uwezo wa nyerere hakuwa nazo...
 
Huwa najiuliza kama kuna kiongoz wa africa aliyekuwa na sifa hata nusu za huyu mtu... Nashangaa hata Mandela alivuma kwa lipi hasa.. Maana hata robo ya sifa na uwezo wa nyerere hakuwa nazo...
Kweli mkuu, uzuri wa historia huwa haifutiki. Kuna siku hili litawekwa sawa for good. Tz inabidi tuchape kazi, tukiongelewa kwa maendeleo na Nyerere atazungumzwa pia. Tumesha anza kuzungumzwa ni swala la muda tu.
 
Kweli mkuu, uzuri wa historia huwa haifutiki. Kuna siku hili litawekwa sawa for good. Tz inabidi tuchape kazi, tukiongelewa kwa maendeleo na Nyerere atazungumzwa pia. Tumesha anza kuzungumzwa ni swala la muda tu.
Unajua watu hawajui umasikin wetu unatokana na nguvu kubwa ya rasilimali ya nchi kutumika kupigania uhuru wa mataifa karibia 12ya africa .. Ukifustilis uchumi wa east africa kabla ya 1970 kenya na tanzania zilikuwa ns uchumi almost sawa.. Ila vita ya uganda na tanzania ilitumia hela nyingi sana ikaacha azina ikiwa empty..

Ajabu baadhi ya mataifa yanayo tuzunguka yana tuchukulia poa kuwa nimasikin lakin hawajui uhuru wa nchi zao umetugharimu sana.. Ila yote kwa yote kuna baraka mungu katupendelea saana nayo ni amani na umoja.. Wanao tucheka wao ndani kwa ndani wanachekana pia na wana baguana..
 
Ubongo was nyerere ulikua sio was kawaida, natamani nijue IQ take ilikua ngapi ila naona Alikua a Gift from God. Mungu alimuumba hivyo ili aje kukomboa waafrika Na alifanya.
Sina cha kumlipa ila mwanangu mmoja atachukua jina lake.
 
Tunamsifu kupita kiasi utadhani hakuwahi kufanya makosa
 
Huyu ndo Baba wa taifa kweli sio kama wa nchi mmoja Afrika Mashariki ambae anakubalika na kuenziwa na kabila lake tu .
 
Kapoteza, kawaweka vizuizini watu wengi sana katika utawala wake.
He was not that innocent.
 
hongera zakew mzee ila alifeli na vijiji vyake vya ujamaa!
 
...14. Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km)
and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region, Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania...
Ongeza Julius Nyerere Crescent, Asokoro, Abuja Nigeria.
 
Unajua watu hawajui umasikin wetu unatokana na nguvu kubwa ya rasilimali ya nchi kutumika kupigania uhuru wa mataifa karibia 12ya africa .. Ukifustilis uchumi wa east africa kabla ya 1970 kenya na tanzania zilikuwa ns uchumi almost sawa.. Ila vita ya uganda na tanzania ilitumia hela nyingi sana ikaacha azina ikiwa empty..

Ajabu baadhi ya mataifa yanayo tuzunguka yana tuchukulia poa kuwa nimasikin lakin hawajui uhuru wa nchi zao umetugharimu sana.. Ila yote kwa yote kuna baraka mungu katupendelea saana nayo ni amani na umoja.. Wanao tucheka wao ndani kwa ndani wanachekana pia na wana baguana..
Nyie husema Kenya ilijengwa na mkoloni, iweje sasa unakubali uchumi wetu ulikua sawa kabla ya 1970.
 
Back
Top Bottom