Mwl Julius Nyerere

Mwl Julius Nyerere

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13 April 1922 na alifariki tarehe 14 October 1999, alikuwa rais wa Tanzania alieongonza nchi ambayo ilijulikana kama Tanganyika kabla. 1964 Tanganyika iliungana na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Nyerere alikuwa rais kutoka 1960 Tanganyika ilipopata uhuru kutoka kwa msimizi wake wa maswala ya utawala Uingereza mpaka kustaafu kwake 1985.

Nyerere ni mtoto wa Chifu Nyerere Burito ambae alikuwa Chifu wa Wazanaki, alizaliwa 1860 na kufariki 1942. Jina linalojulikana sana kwa Nyerere ni Mwalimu hii ilikuwa taaluma yake kabla ya kuwa mwanasiasa. Nyerere alisoma katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala na Chuo Kikuu cha Edinburgh Scotland kabla hajarudi Tanganyika ambako alifanya kazi kama mwalimu. 1954 akisaidiana na wenzake waliunda chama cha siasa kilichojulikana kama Tanganyika African National Union (TANU).

Wakati Tanganyika ilipopewa madaraka ya kiserikali mwaka 1960, Nyerere alikuwa Waziri Kiongozi na aliiongoza Tanganyika kufikia uhuru mwaka mmoja baadae na kuwa alikuwa Waziri Mkuu mpya. Nchi ilikuwa Jamhuri mwaka 1962, na Nyerere akiwa rais wa kwanza. Kipindi hiki Nyerere aliunda serikali ya chama kimoja, serikali hii ilipabana sana nguvu za vyama vya wafanyakazi kueneza vuvugu la kisiasa. Baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibara 1964, mwaka uliofuatia kulikuwa na uchaguzi mkuu 1965 na Nyerere alikuwa mgombea pekee, aliendelea kuchaguliwa bila kupingwa mpaka mwaka 1985 alipostaafu.

Mwaka 1967, alikuwa kwenye ushawishi mkubwa wa Ujamaa wa Afrika, Nyerere alipitisha Azimio la Arusha, ambalo lilikuwa na maono na ujamaa. Ujamaa ni mfumo ulioongoza katika sera za Nyerere. Hata hivyo sera hizi ziliendea kushuka kwa uchumi, rushwa na bidhaa kupotea makudani. Mwanzoni mwa miaka ya 1970, Nyerere aliamuru majeshi kuhamisha watu kuelekea katika vijiji vya ujamaa, sera hii ilipingwa na wengi, vijiji vilichomwa moto. Kampeni hii ilisababisha njaa katika nchi na ililetea nchi kutegemea msaada wa chakula kutoka nje. Huu ulikwa wakati wa ugali wa Yanga, uji wa bulger kwa wale waliokuwepo.

Mwaka 1985, baada ya zaidi ya miengo miwili kama rais, aliachia madaraka na kumchagua aliyemfuatia Ali Hassan Mwinyi. Nyerere aliiacha Tanzania ikiwa nchi masikini sana, nchi iliyokosa maendeleo na nchi iliyotegemea misaada kutoka nje ingawa katika huduma za jamii kama elimu, afya na vingivevyo alifanikiwa sana. Nyerere bado ni jina lenye ushawishi mkubwa Tanzania hata baada ya kifo chake kilichosababishwa na leukemia mjini London 1999.

Maisha ya awali ya Nyerere.
Kambarare Nyerere alizaliwa 13 April 1922 katika kijiji cha Butiama Tanganyika wakati huo Mkoa wa Mara. Alikuwa mmoja wa watoto 26 wa Chifu Burito Nyerere. Alianza elimu katika shule ya serikali Musoma akiwa na umri wa miaka 12 ambapo alimaliza elimu ya darasa la nne katika miaka mitatuhapa hata walimu wake waliuona uwezo wake mkubwa darasani. Baada ya hapo alikwenda shule ya serikali ya Tabora 1937. Wakati huo Tabora ilikuwa shule bora sana kwa elimu na alibatizwa kwa imani ya Kikatoliki na kuitwa Julius.

Alipata nafasi ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Makerere mjini Kampala, Uganda. Akiwa pale alianzisha chama cha Tanganyika welfare Association, ambacho kilikuja kuungana na Tanganyika African Association (TAA), ambacho kilianza mwaka 1929. Nyerere alipata diploma ya ualimu mwaka 1947. Alirudi Tanganyika na kufanya kazi kwa miaka mitatu shule ya Sekondary ya Mtakatifu Mary Tabora, ambako alifundisha Biology na Kiingereza. Mwaka 1949 alipata nafasi iliyodhaminiwa na serikali kwenda kusoma katika Chuo Kikuu cha Edinburgh. Pale alipata Shahada ya uzamili katika masomo ya sanaa katika Uchumi na Historia mwaka 1952. Akiwa Edinburgh alikutana na Fabian Society ambayo ni Jumuiya ya Waingereza waliokuwa na nia ya kueneza siasa za kidemokrasia kwa misingi ya ujamaa. Nyerere alianza kuunganisha siasa za ujamaa na jamii za Kiafrika na enzi za ujima.

Maisha kama mwanasiasa.

Aliporudi Tanganyika, Nyerere alianza kufundisha Historia, Kiingereza na Kiswahili, katika shule ya sekondary ya Mtakatifu Francis (baadae illitwa shule ya sekondari Pugu), nje kidogo ya jiji la Dare es Salaam. 1953 alichaguliwa kuwa mwenyejiti wa Tanganyika African Association (TAA), shughuli ambazo alizianza tangia akiwa Makerere, mwaka 1954 alikibadilisha TAA kwa Tanganyika African Nationa Union (TANU). Nia kubwa ya TANU ilikuwa kuleta uhuru wa Tanganyika. Kampeni za kuingiza wanachama wapya zilizanza na katika kipindi cha mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa chama kikuu cha kisiasa katika nchi.

Katika mihangaiko hii ya Nyerere, serikali ya Kikoloni ilianza kuwa na tahadhari, aliitwa na kuamrishwa achague kimoja kati ya siasa au taaluma yake ya ualimu. Alinukuliwa akisema "kuwa mwalimu ilikuwa uamuzi lakini siasa ni ajali". Alijiuzuru kama mwalimu ili aweze kuzunguka Tanganyika nzima akiongea na wananchi pamoja na viongozi wa jadi (machifu) wa makabila tofauti akijaribu kupata ushirikiano katika jitihada za kupata uhuru.

Alongea pia kama mwakilishi wa wananchi wa Tanganyika katika baraza la umoja wa mataifa juu ya Uangalizi wa Uingereza huko New York. Nyerere alikuwa na uwezo mkubwa wa kujenga hoja zilizovutia waliomsikiliza, na hii ilimsaidia sana katika jitihada zake za TANU kuipatia Tanganyika uhuru bila kumwaga damu. Bwana Richard Turnbull ambae ndiye alikuwa mwakilishi wa serikali ya Mwingereza Tanganyika (Governor) wakati huo pia alikuwa chachu ya kupatikana kwa uhuru. Nyerere aliingiia katika Bunge la mkoloni katika uchaguzi wa 1958-1959 na alichaguliwa kama waziri kiongozi kabla ya uchaguzi wa 1960.

Manamo 09 December 1961, Tanganyika ilipata uhuru na kuwa moja ya nchi za Jumuiya ya Madola na Nyerere akawa Waziri wake Mkuu wa Kwanza. Mwaka mmoja baadae Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa Tanganyika ilipokuwa Jamhuri. Mwezi mmoja baadae alitangaza kuwa madhumuni sasa sio kuwaunganisha watu na kufuatilia uchumi, TANU sasa ndio chama pekee cha siasa kinachotambulika. Tangia hapo, serikali imekua ikiendeshwa wa mfumo wa chama kimoja tangia nchi inapata uhuru. Nyerere alitafsiri maandishi ya Shakespare juu ya Julius Caesar kwa Kiswahili kama zawadi ya nchi kusherehe wa uhuru.

Nyerere ndiye aliyekuwa dhana ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuwa Tanzania, baada ya mapinduzi ya Zanzibar 12 January, 1964 ambayo yalimtoa Sultan wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah. Kiongozi wa mapinduzi hayo alikua mwanaume wa kazi John Okello akitokea Lira Uganda, ambae alidhamiria kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Nyerere alistushwa na jaribio la kupindua serikali siku chache baada ya hapo, alihakikisha Okello harudi Zanzibar baada ya kutembelea bara.

Ingawa uzi huu unamhusu Mwalimu ngoja niongeze kidogo kuhusu John Okello, yeye ndiye alieyefanikisha Mapinduzi ya Zanzibar na baadae kiongozi wa Afro-Shiraz Party; Abeid Karuma kuwa rais wa kwanza na aliyekuwa kiongozi wa chama cha Waarabu Umma-Massa Party Sheik Abdulrahamn Muhammad Babu kuwa waziri Mkuu na baadae Makamu wa Rais. Hakuna hata mmoja kati ya hawa alikuwepo wala hawakujua kinachoendelea kuhusu mapinduzi. Hata hivyo kati ya Karuma na Babu hakuna aliyetaka kushirikiana na Okello kwa jambo lolote. Okello alikukuta katika wakati mgumu kuwa kwenye serikali mpya ambayo yeye hakuwa na nafasi yeyote. Karume ndiye aliyeonekana na nguvu kubwa katika madaraka na maamuzi yote na baadae aliamuru Okello aendelee kubaki Zanzibar akipewa cheo cha Field Marshal

Ilipofika 03 February, hali ya Zanzibar ilikuwa shwari na Karume aliikubali kuwa rais, na Okello aliunda jeshi lililojulikana kama Freedom Military Force (FMF), kutokana na watu waliomuunga mkono. Walizunguka mitaani kutuliza ghasia, kutokana na ukakamavu na roho ngumu aliyokuwa nao Okello na Kiingereza chake chenye laufidh nzito ya Acholi, na yeye kuwa Mkristu alionekana kituko kwa Wanzazibar. Ilipofika March jeshi la FMF lilianza kupungua nguvu kutoka na waliomuunga mkono Karume pia wafuasi wa Umma Party. Okello hakuruhusiwa kurudi tena Zanzibar alipokuwa anatoka safari, alipelekwa Tanganyika baadae Kenya kabla ya kurudi kwao Uganda. Nafasi yake ya u Field Marshal ilifutwa rasmi 11 March.

Baada ya hapo jeshi la wananch liliundwa (People's Liberation Army PLA) jeshi hili lilimaliza kabisa nguvu za John Okello na haikukuchukua muda Karume akatangaza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Sababu za Karume kujiunga na muungano ilikua kuzuia wanasiasa wenye siasa kali wa Umma Party kuchukua madaraka zaidi ya nchi kwakua walishaanzisa siasa za ujamaa. Hata hivyo agenda nyingi za Umma Party ndizo zilizoendelea kuongoza nchi hasa kwenye upande wa elimu, afya na ustawi wa jamii.

Akiwa madarakani, Nyerere alipitisha Azimio la Arusha, ambalo liliazimia kuleta uchumi wa kujamaa. Pia alianzisha urafiki wa karibu na Watu wa Jamhuri ya China chini ya rais wao Mao Zedong. Mwaka 1967, makampuni mengi yalibifasishwa na serikali kuwa mwajiri mkubwa. Karibu kila kitu kilimilikiwa na serikali, kuanzia uingizaji wa bidhaa nchini na uuzaji wa bidhaa nje, hata uokaji wa mikate, hali hii ilikaribisha uhujumu uchumi na ubadhrifu wa mali ya umma.

Biashara za watu binafsi ziliathirika sana, usumbufu na taratibu nyingi zilizotakiwa kukabilishwa pia kodi. Pesa nyingi za umma zilitumika kwa shughuli ambazo hazikuzalisha. Nguvu ya manunuzi ilipungua na hata bidhaa muhimu madukani zilipotea. Utaratibu wa kupata kibali karibu kwa kila kitu, hii ilipelekea waliofanya kazi maofisini kuchukua rushwa ili watoe vibali. Viongozi wa chama walikuwa na mabenzi na kulikuwa na usemi wa "wabenzi". Mfumo ulikuwa ni msingi wa rushwa iliyoendelea kwa miaka mingi baadae.

Ujamaa ulikuwa umeshika kasi iliopofika 1971. Kwasababu watu wengi waliupinga, nguvu ya dola ilitumika kuwahamisha watu kwenda kwenye vijiji vya ujamaa. Nyumba zilichomwa moto na kuharibiwa na mali za watu kabla ya ujamaa ziliharibiwa. Wasiokubali kuhama hawakupata mgao wa chakula. Mali nyingi na mashamba ya matunda, na mazao mengineyo yaliachwa yakiharibika. Mifugo mingi ilipotes, kuugua, iliibiwa au ilikufa.

Wakulima wadowadogo waliwezesheshwa sana katika kilimo, pembejeo zilitolewa na vipindi vya ukulima wa kisasa vilifanisha sana kuwaelimisha wanavijiji. Mazao yaliyopewa kipaumbele yalikuwa chai, tumbaku, pamba na kahawa. Kwa mara ya kwanza ile imani ya chai kulimwa kwenye mashamba makubwa ilipotea. Matokeo yake uhaba wa nafaka uliivaa tena nchi. Kingine kilichoharibu uchumi ilikuwa vita ya Uganda, baada ya hapo bidhaa kama dawa ya meno, betri, sukari, khanga na vitenge vilikuwa adimu madukani.

Katika kipindi hiki pia elimu ya msingi ilipanuliwa na kulikuwa na mfumo wa elimu kwa wote (Universal Primary Education), nia ikiwa kila mtoto wa Kitanzania ajue kusoma na kuandika na ahitimu darasa la saba. Mafunzo ya ualimu yalitolewa kwa waliomaliza darasa la saba walipewa mafunzo mafupi ya kukidhi mahitaji ya walimu kwa darasa la kwanza mpaka la nne, wakati waliomaliza darasa la kumi na mbili walifundisha darasa la tano mpaka la saba. Elimu ya watu wazima pia ilisaidia wale waliokosa nafasi ya kujifunza kusoma na kuandika. Kwa kifupi uwezo wa watu kusoma na kuandika Kiswahili serikali ilifanikiwa sana.

Uhasiano na mataifa ya nje.
Sera za nje za Nyerere zilikuwa za kutokufungamana na upande wowote. Wakati vita baridi ikiendelea kwa mataifa ya Magharibi, uongozi wa Nyerere ulikuwa na uhusiano mzuri sana na Jamhuri ya watu wa China pamoja na nchi za Soviet.

Nyerere alitangaza Tanzania kuwa nchi ya kwanza kuitambua Biafra mara tu baada ya kujitangaza kuwa wako huru kutoka Nigeria, lakini kwa hili alilaumiwa kwa kutoishirikisha serikali yake, hii pia ilileta msuguano wa kimahusiano na Nigeria.

Nyerere pamoja na wenzake waliunda kundi la viongozi lililojulikana kama Pan-Africa, walianzisha Organisaton of African Unit (OAU) 1963. Nyerere alisaidia vikundi vingi vya mapambano ya kupata uhuru wa Afrika, kikiwemo African National Congress (ANC) na pan Africanist Congress cha kusini mwa Msumbiji, pia FRELIMO kilipoanza harakati za kuwatoa Wareno, MPLA kilipoanza kuwatoa Wareno Angola na ZANLA kilipokuwa kwenye vita na Smith wa Rhodesia ambayo sasa ni Zimbambwe. Kuanzia katikati ya miaka ya 70 pamoja na rais Keneth Kaunda alikuwa kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa Afrika na kutokomeza ukoloni. 1978 Tanzania iliingia vita na Uganda na matokea yake ilimtoa Idi Amin kutoka madarakani.








alow
witnessj
 
Thanx my dear kwa kuniita...hivi huyu Mzee (nyerere) ndo anamzaa huyu anayepostigi humu JF?
 
Back
Top Bottom