Si vbaya kwa sababu tangu wakoloni wanaingia na kuanzisha tawala zao kulikuwa na vugu vugu la kuwapinga kutoka kwa Machifu na Viongozi wa makabila km Mkwa- Wahehe, Songea - Wangoni, Mirambo - Wanyamwezi. Baada ya Mwal. Nyerere kuanza harakati akaona na vizuri wote waunganishwe na kudai uhuru kwa pamoja kama nchi kuliko kabila moja moja. Hata Mwal. Nyerere na Kwame Nkrumah walikuwa na mwono wa kuwa na Afrika moja, lakini kila mmoja alipigania uhuru wa chi yake kwanza. Kwa hiyo huyo Mangi anapaswa kupongezwa kwa kukubali maoni ya Mwal. Nyerere, hakuna sehemu katika historia inayoonyesha kuwa huyo Mangi alikataa kumwuunga mkono. Ni swala la kupongezwa badala ya kubezwa, vinginevyo, angeweza kukataa na kuendelea na kudai uhuru wa Kilimanjaro pekee kitu ambacho kilikuwa kinapendwa na wakoloni katika mfumo wa "Divide and rule".