Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 961
- 533
Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya makimu kuhukumu kesi kwa matakwa yao na kuacha kuzingatia weledi. Utakuta mshtakiwa anakuwa amefanya kosa ambalo angestahili afungwe labda tuseme miezi 3 au alipwe faini ya tsh 50000/= Lakini kutokana na kukosa uweledi hakimu anatoa hukumu ya mtuhumiwa kufungwa mwaka mmoja ndani. Mtuhumiwa akikata rufaa kupitia wakili wake, kesi hiyohiyo ikahukumiwa na hakimu mwingine anabatilisha hiyo kesi na kuonekana kuwa hakimu wa kwanza alikosea kuisoma ile hukumu na kwamba kwa mujibu wa kosa alilofanya mtuhumiwa, hukumu yake labda tusema ni faini tu ya tsh elfu 50 au kifungo cha miezi 3.
Nataka kujua ni nini hukumu inayotolewa na majaji wasiozingatia weledi?
Nataka kujua ni nini hukumu inayotolewa na majaji wasiozingatia weledi?