Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261
Unapotafuta kununua gari iliyotumika (used/second), uamuzi wa kujua gari ipi itakufaa utategemea mahitaji, bajeti, na mapenzi yako binafsi. Haya ni baadhi ya maswali yanayoweza kukuongoza kufikia maamuzi sahihi:
Je, una bajeti ambayo haiwezi kuongezaka?
Maswali kama hayo yanaweza yakakupa pa kuanzia.
- Je, itakuwa ni gari pekee au una gari nyingine ambalo litakuwa na matumizi madogo au sawa au litatumika mara kwa mara?
- Je, utakuwa ukitumia gari kwa safari fupi au ndefu za mara kwa mara?
- Je, una wazo lolote kuhusu umri wa gari unalolihitaji au umbalo ambao lishakwisha tembea?
- Je, una upendeleo wowote wa kampuni ya gari (mfano Toyota, BMW, Land Rover n.k.) au aina ya gari (mfano Prado, Range Rover n.k) au rangi?
- Je, unategemea kubeba watu wangapi kwa wastani?
- Je, wataka nafasi ya ziada nyuma ya gari ili kubeba vitu vya ziada?
- Je, wapendelea gari zilizopanda juu?
- Je, vitu gani vya gari vina umuhimu zaidi kwako vilivyotajwa hapo chini?
- Usalama
- Matumizi ha mafuta
- Ukubwa wa gari
- Idadi ya milango ya gari
- Gharama za kuliendesha gari ikiwa pamoja na upatikanaji spare na mafundi
- Gharama za bima
- Four wheel
- Gharama za kununua gari
- Uzoefu wa kuliendesha
- Nafasi ya ndani
- Nguvu ya gari
- Thamani yake ukitaka kulituma tena (Resell value)
- Vikorombwezo uvitakavyo kwenye gari
Je, una bajeti ambayo haiwezi kuongezaka?
Maswali kama hayo yanaweza yakakupa pa kuanzia.