INCHI kwa sasa inamuogopa mtu mmoja tu imrfika point watu wanakana hadi taaluma zao ili wateteee uongo wa mtu mmoja.Madaktari “hawajui” jina la ugonjwa lakini muongozo wa kutibu wanaujua!
Wimbi lapili lilipoibuka wananchi wangepewa taarifa mapema ili wale waliokwenye makundi hatarishi wangejilinda na maisha mengi yangeokolewa. RIP wote hao.
Sasa jamani na nyie madaktari tena madaktari bingwa si mseme tu Covid 19.Mmeshakuwa wanasiasa sasa.Madaktari mlituambia kuwa ni nimonia,mkatuambia tena, sasa mnakuja na mfumo wa upumuaji.Covid 19 ni sawa na magonjwa mengine kama ebola nk.msiogope kutuambia ili tuchukue tahadhari.Kwa mujibu wa chama cha madaktari nchini MAT kimeandaa jopo la madaktari bingwa ili kutoa mwongozo namna wagonjwa wanaoumwa mfumo wa kupumua wapate tiba ya namna gani...
Huu upuuzi wa nyungu hapanakama wanaogopa kutaja jina la ugonjwa basi hata huo muongozo wao ni feki siyo wa kuuamini. Bora tuendelee kupiga nyungu kwa kasi mpya!
Hao Madaktari wamekubali kugeuzwa kuwa Waganga wa kienyeji bila shaka! Sasa ugonjwa wa kushindwa kupumua na kushauriwa kunawa mikono, wapi na wapi!Nimeona mkurugenzi wa kinga amejizuia katakata kutaja barakoa kwenye kinywa chake kama kinga ya corona bali anasema watu wanawe mikono
Woga ni kitu kibaya sana, viongozi wote waandamizi hakuna anayevaa barakoa wakiogopa kutumbuliwa.Hao Madaktari wamekubali kugeuzwa kuwa Waganga wa kienyeji bila shaka! Sasa ugonjwa wa kushindwa kupumua na kushauriwa kunawa mikono, wapi na wapi!
Si wanyooshe tu maelezo ya kwamba Corona imetamalaki mtaani ili mapambano dhidi ya huyo mdudu yapambe moto!!