Mwongozo wa Namna ya Kuanzisha na Kuendesha Biashara ya Mini Supermarket

Ashangedere

Senior Member
Joined
Aug 9, 2010
Posts
119
Reaction score
32


Habari wangudu,

Nimeona niweke hapa business idea yangu ya kufungua retail shop in one on the medium populated areas hapa dar.

Nataka kufungua duka ambalo litakuwa na groceries (eg mafuta ya kupaka & kupika, unga, nido kahawa pampers,maziwa fresh, soda mikate, nk). Maeneo ambayo nimepanga kufungua ni kwenye barabara kuu katika sehemu ambazo zimejengwa karibuni au zinaelekea maeneo yaliyojengeka karibuni, kama mbezi, kimara, afrikana, tank bovu njia ya goba etc..

Mara nyingi wanaishi watu ambao ni proffessionals, unakuta wana kausafiri na familia na wanaishi katika nyumba zao binafsi, watu hawa kwa mtazamo wangu ni wateja wazuri wa groceries wakati wakiwa wanarudi kutoka kazini wanaweza pita na kununua mahitaji, vipi great thinkers

Mnaonaje kuhusu hii idea yangu? mimi pia ni muajiriwa na ni mteja mzuri wa aina hiyo ya maduka na nimefanya kasurvey kangu nimeshagundua eneo zuri. Mnaonaje kuhusu hii business na kwamba nitaweka watu na sio mimi nitakuwa dukani, mimi nitakaa siku za weekend tu.

Nawakilisha.

WADAU WENGINE WANAOPENDA KUJIFUNZA BIASHARA HII
Naombeni ushauri,

Nina mil 5 je naweza fungua mini Supermarket. Nipo Arusha, pia naomba kujua kama nikifungua bidhaa nachukulia wapi?

Mawazo yenu please!


USHAURI/MICHANGO YA WADAU


Biashara ya supermarket ndogo (Mini Supermarket)​

Enzi hizo biashara za supermarket wanunuzi wake walikuwa wachache wenye kipato cha ziada ila kwa sasa supermarket zimekuwa zikipata wateja wa kila aina. Tafiti zinaonesha kuwa katika kila watu kumi wa mijini watu watano hupendelea kununua bidhaa katika supermarket (ama angalau mini supermarket). Mabadiliko haya yametokana na kuzagaa kwa supermarket kila kona na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata kipato cha kati. Hivyo basi, kuazisha mini supermarket kwaweza kuwa wazo zuri sana la kibiashara endapo una mtaji wa kutosha kuweka kila kitu ndani yake. Acha leo niongelee jinsi unavyoweza kuanzisha mini supermarket yako mwenyewe. Sitoongelea supermarket kubwa bali zile ndogo ndogo.

ENEO:
Ndani ya Dar es Salaam, mwanza ama arusha, kupata eneo linalotosha kuweka supermarket ndogo unahitaji kati ya Tshs 800,000 hadi 3,000,000 kutegemea na ukubwa wa chumba cha biashara na wingi wa watu katika eneo husika.

Kuna msemo huwa naupenda sana. Msemo huo si mwingine bali ni ule usemao “Vidogo Vyavutia”. Tuchukue hiki kiwango cha chini cha Tshs 800,000. Tunalipa miezi sita inakuwa Tshs 4,800,000. Mh, acha kuguna. Usije ukaogopa mpaka ukaacha kuwaza kuanzisha biashara hiyo. Jua kuwa asilimia kubwa ya pesa utayolipa kwenye mini supermarket ni kodi ya upangaji.

LESENI NA VIBALI:
Ili kufanya biashara ya mini supermarket unahitaji vibali mbali mbali na leseni. Usiumize kichwa juu ya hili maana hata uendapo ugenini unahitaji kujua nauli za daladala za kule japo hakuna anaejishuhulisha kuulizia. Unachotakiwa kujua ni bajet ya kuandaa kwa nauli za daladala ama texi kule uendako. Ili usisumbuke na suala la vibali na leseni weka bajet ya Tshs 600,000 itamaliza kila kitu.

BIDHAA:
Wapo wasambazaji kadhaa walio tayari kusambaza bidhaa mbali mbali kwenye mini supermarkets. Hawa husambaza mlango hadi mlango. Unahitaji kujiandaa na kati ya Tshs 10,000,000 na 20,000,000 kujaza bidhaa ndani ya supermarket. Kwakuwa “Vidogo Vyavutia” acha tuanze na Tshs 10,000,000.

WATUMISHI:
Kwa supermarket ya bidhaa za milioni 10, hapo wapaswa uwe na watu wasiozidi 5 watakaofanya kwa shift ya watatu watatu. Hawa watakugarimu kama Tshs 2,000,000 kwa mwezi.

FAIDA:
Mini supermarkets hutoa faida kati ya Tshs 2,000,000 na 3,000,000 kwa mwezi. Kwakuwa tumeamua kuanza kile “Kidogo Kinachovutia” faida yetu itakuwa Tshs 2,000,000 kwa mwezi.

CHANGAMOTO:
Huwa hakuna biashara isiyo na changamoto. Changamoto ya kwanza kwa supermarket ndogo ni wizi. Wamiliki wengi wa supermarket ndogo ndogo hulalamikia suala la wizi kutoka kwa wateja na watumishi wao. Ni rahisi mtumishi wako kukwepa wizi wake na kusingizia wateja. Wapaswa kuweka mitego mbali mbali ya kupunguza suala la wizi ili unufaike na faida itokanayo na biashara yako. Moja ya mitego hiyo ni cctv camera. Kwa kawaida ukiweka camera hata mbili tu zitasaidia sana. Hii hugarimu wastani wa Tshs 1,200,000.

Changamoto nyingine ni bidhaa kufikia mwisho wa matumizi (yaani kuexpire). Wasambazaji kadhaa wapo tayari kuchukua bidhaa zinazoisha muda wake japo sio wote. Kupunguza uwezekano wa kupata hasara kutokana na bidhaa kuisha muda wake wa matumiz kabla hazijanunuliwa, jaribu kununua bidhaa zako nyingi kwa wasambazaji walio tayari kuchukua bidhaa zilizokweisha muda wake. Pia jitahidi kununua bidhaa ambazo zimetengenezwa muda mchache ulipita ikiwezakana hata kuwapa masharti wasambazaji kuwa bidhaa zinazozidi mwezi wasikuletee.

Pia kuna bidhaa ambazo hazitouzika kabisa na wapo wateja watakaohitaji bidhaa ambazo wewe hauna. Hii ni changamoto ila isije kukuvunja moyo kwani itakusumbua mwanzoni tu na baadae utakuwa mzoefu.

Biashara ya mini supermarket ni biashara yenye faida sana ila huhitaji mtaji usiopungua Tshs 17,000,000 na uangalizi wa karibu ili kushamiri.

Credits: Juma Kessi/miamia.co.tz
 
Ndugu yangu biashara hiyo ni nzuri lakini faida yake ni ndogo sana hata siku moja huwezi kutoka kwa biashara hiyo, hapo sanasana utapata hela ya kula tu, kama utaweka na vivywaji kama bia unaweza kupatapata kidogo,halafu kitu ulichoharibu kabisa uliposema utaweka watu ndio nimesita kidogo manake biashara za sasa hivi kama uko siriaz.

Unahitaji kusimamia mwenyewe na familia yako manake kama unasema kuweka watu baki basi utakua unataka kutajirisha watu wengine, ndio maana unakuta wahindi wanatajirika sana manake hata siku moja hawafungui biashara na kuacha watu hapo wao wakaendelea na shughuli nyingine.

Wanafungua biashara baba, mama watoto wote wanakua madirector wanasimamia biashara zao, lakini ukisema unafungua duka halafu unaachia watu unakwenda kazini utakua unatajirisha wengine na biashara hiyo itaakufa mara moja.
 
USHAURI MUHIMU

Nafikiri biashara yako lazima iende na vitu kama soda na bia au pombe ambazo zinanunulika sana kwa Tanzania. Pia vyakula vinakwenda sana ila sema upate sehemu utakaponunua kwa bei nafuu na wewe bado uuze kwa bei nafuu. Ila si lazima uige wengine wanafanyaje. Unaweza kuja na mipango mipya na ukaanzisha biashara ya aina ya pekee. Labda tu itabidi ukae sana na kufikiria. Nenda kwenye maduka angalia wengine wanafanya makosa wapi na wewe unaweza wapo kurekebisha.

Wauza duka wana nafuu zaidi Wanawake. Wanaume watakuliza sana kwani wengi hao hasa vijana huwa kasheshe. Labda uweke vyombo vya kusoma kila bidhaa inayotoka dukani inabidi kuifuta SUMAKU yake vinginevyo inapiga kelele. Nguo wanakuwa na miblastic ambayo inaidi kimashine chake kufungua. Ila hivyo vyombo sasa shida ya umeme utalia. Pia kama kuna Camera na vioo. Ila Counter bado wanaweza kukuliza tu. Itabidi kwa hilo ujipange uone wengine wana solve vipi.

Kama utahitaji PERFUMES basi niye nauza aina kadhaa kwa bei nzuri sana na natafuta wenye maduka. Ukilinganisha ubora na bei, utakuta kwamba bei yake ni rahisi sana. Karibu sana ukitaka kushirikiana na sisi na kila la kheri katika biashara zako.
 
Aina ya biashara ni nzuri kama iko sehemu yenye wateja wazuri. Tatizo la biashara ya aina hiyo ni gharama za uendeshaji kuwa kubwa na pia parishable food kutupa huleta hasara. Biashara aina hiyo hata nchi za majuu kinachowaingizia pesa ni tobacco, alcohol na soft drink. Lakini chakula tu wengi hupendelea kununua supper market.

Kumbuka kivutio cha biashara kama hiyo unatakiwa uwe na commercial coolers kwa ajili ya vinywaji, na baadhi ya vyakula ili kuwa na kiwango kinachohitajika kwa stage ya watu ambao wamekuwa umeeleza. Sasa Umeme huu wa mgao MHHHHHHHHHH
 
Ndg wana JF ni matumaini yangu mu kheri wa afya njema.

Naomba USHAURI juu ya biashara ya Min Supermarket kama italipa, mtaji wangu sio zaidi ya 10M.

Naomba wenye ufahamu na hiyo biashara kama kila bidhaa au bidhaa zote ndani ya supermarket huwa zinanunuliwa na mmliki wa supermarket? (do i have to buy everything to put in my ka small supermarket?)

Pia kuna mtu kaniambia bidhaa ndani ya supermarket huwa zinabadilishwa na kuwekwa zingine mpya kila baada ya miezi kadhaa, je hiyo ina ukweli ndani yake?

Mie ni mzoefu wa biashara za madukani (retail shops) kwa mda mrefu.

Wenu ktk ujenzi wa Taifa la TANGANYIKA.
 
What I know ni kwamba Mini supermarket inalipa bila longo longo.

Kwa mtaji wa Milioni 10 hautoshi, labda kama tayari umeshapata jengo na ujenzi wa flemu za kupangia bidhaa umeshafanyika then hiyo 10Mil ni ya kununulia bidhaa, hapo itatosha.

Kikubwa ni location.

Tumia muda wako mwingi kufanya utafiti wa location kwani ukikosea hapo kila kitu kitaharibika.
 
try to outsource contract suppliers/producers like cadbary for chocolate, azam products, del monte,uniliver, brookside, coca cola, etc , you will save from their bulk resale/wholesale price and good enough the products will be delivered at the door of your shop theirfore increase your profit margin by saving transportation costs, also their products are quaranteed incase of technical defects and your shop will enjoy seasonal sales by swapping/exchange of slow moving product to fast moving goods from above mentioned dealers

pia utapata marketing and promotional materials free from these companies, the likes of tshirts, caps, plastic bags, pen, umbrellas, flyers and posters that market and advertise the products at your shop free
 

Nakubaliana na ushauri huo, lakini shaka langu ni kwenye bidhaa ambazo ni parish-able food, hapo ndipo maana si kila mara zote zitanunuliwa, ndio maana utaona bidhaa za supermarket ni kubwa kwa ajili ya kufidia bidhaa ambazo huharibika mapema na kutupwa. Wasambazaji wengi wa bidhaa hizo hawana garantee ya kubadilisha zilizoharibika hasa katika nchi nyingi za Afrika.

Kwa vyovyote fanya utafiti wa kutosha kabla hujaanza, maana wengi hapa tutakupa maumaini halafu baadaye ukaona mambo ni kinyume chake. Usitegemee zaidi ushauri wa hapa, bali ushauri wetu utakusaidia kupata majibu sahihi katika utafiri utakaofanya kwe wenye uzoefu na bishara za aina hiyo hapa Tanzania.
 
Njela

Your comments/advice/opinion and views are highly valued
 

Ongezo: chukua muda kutafiti vitu vinavyotakiwa, ili viweze kutoka vikinunuliwa.
 
Hapo unamtihani sana mtaji mdogo eneo la watu wenye tamaduni wa ununuzi kwenye super market yanataka mtaji mkubwa kwa maana akija akitaka item anapata za kumtosha so hichi huna kile huna, ila kikubwa ubunifu ndo utaweza, ubunifu wako ndo utakufanya umudu biashara hiyo.
 
Mkuu kwangu mm supermarket ni kimeo!expiring ndio changamoto!unaeza kuta bidhaa zina expire karibu za milion 2 kwa mkupuo! Inabd uwe very strategic kwenye supermarket mkuu!otherwise utalia kama Patcco.
 

UZOEFU KUHUSU BIASHARA HII

Supermarkets zinaushindani sana kwa makampuni makubwa, hata hivyo makampuni mengi siku hizi yanafunga supermarkets zao kutokana na hasara kubwa wanayopata. Kwa mazingira ya Tanzania tunahitaji supermarkets chache kwa sababu wengi wetu hawapendelei kununua huko kwa sababu ya nchi yetu bado haijawa industrialized. Vyakula ambavyo havijawa processed ndivyo vyenye soko kubwa kuliko hivi vya supermarket ambavyo vingi vimeshakuwa processed, na mapokeo ya wengi wa kiwango changu tunaogopa vyakula vya aina hivyo kwa kuhofia madawa yatumikayo kuzindikia na kuhifadhia kuathiri afya kama kansa nk.

Kuharibika kwa bidhaa nyingi ambazo ni parishable food kama alivyodokeza mmoja hapo juu ni jambo muhimu kulitilia maanani. Vyakula vingi kwenye maduka aina hiyo huwa ni vya muda vinavyodumu kwa siku au majuma kadhaa na vichache kwa miezi kadhaa, hivyo kujikuta vyakula vingi ukivitupa na hivyo kuongeza bei ya bidhaa zako ili kufidia vile unavyotupa kutokana na kuisha muda wake kutotumika zaidi kiafya. Ughali wa bidhaa utawafanya wateja wabadilili mwelekeo afadhali kwenda Kariakoo, Manzese, nk ambako wanapata organic food for cheap. Kwa kiwango cha biashara hiyo hata mayai yanatakiwa yawe na muda maalum wa kuyauza si kama waswahili tulivyozoea. Ingawa nchi zilizoendelea vyakula hivi vya organic tuanvyoviuza kwenye masoko ya kienyeji ni bora zaidi na ni vya bei mbaya, wenye uwezo tu ndio wanaomudu. Tofauti ya bongo machungwa toka Afrika kusini yana bi ghali ambayo si bora kama yetu ambayo ni organicyanayouzwa kwa bei ya kutupa

Ushauri wangu kwa mazingira ya sasa ya Tanzania, bora kuwa na groceries ambazo vyakula vyake ni vichache na unaweza kumudu na kujua wastani wa wateja wako utakaokuwa nao, vinginevyo unaweza jikuta umeingia hasara kubwa sana, na kujutia kupoteza mtaji wako.

Unaweza kuona na kujifunza jinsi dunia ya leo soko la bidhaa za wese la kuendesha motokaa, ndege na mitambo linazidi kuumiza na wengi wanaamua kuachana nalo hasa mtaifa makubwa, tanzania bado tunalalamika tu kwa sababu ya kutojua halihalisi yanayoendelea katika soko la dunia cause and effect yake, kwaa wafanya biashara waliozoea kutengeneza super net profit na mazingira ya watumiaji kwa sasa v/s wazalishaji. Hali hiyo leo imebadilika ghafla.

Mwisho gharama za uendeshaji wa supermarket ni kubwa sana kutokana na baadhi ya vyakula kuhitaji matunzo ya pekee kama kuwa na coolers ambazo zitakuingizia bills kubwa ya matumizi ya umeme. Utahitaji wafanyakazi wengi zaidi ili kuweza kumudu kuiweka sawa supermarket yako. Kwa vyo vyote si kujiingiza kichwa kichwa, bali fanya utafiti wa kutosha wa eneo, kiwango cha wateja walengwa, makampuni yatakayo supply vyakula hapo ya ndani na nje (vendors). Na mwisho usikose kupata ushauri kwa idara ya afya ya mji unakotaka kuanzisha biashara yako maana biashara hiyo si kama yacorner kiosk, biashara hiyo ina taratibu na sheria zake kutokana na kiwango na ukubwa wake kukithi masharti ya leseni unayokusudia.
 
Soma hapa

If you want to start a business here are the basic ground rules I recommend:

1) Don't go in debt to start a business and have very good credit

2) Work for someone else then do it yourself, journal the successes and failures of the business you are working for and work there a full year so you can note seasonal changes with customers and revenues

3) Always do something on the smallest scale possible before making a huge commitment. Example if you want to open a bakery try selling your baked goods to a local coffee shop first and then get feedback.

4) Try to avoid business partners when ever possible

[h=3]Source(s):[/h]Self employed for over a decade, I start companies up and sell them off, I am on my sixth business right now currently running two companies at the same time with my spouse
 

Wanachokijadili hapa ndicho nilichokisema hapo juu, ni kweli kabisa, hii biashara kichaa sana usipokuwa mwangalifu. Mataifa ya nchi za magharibi unaweza kuona biashara hizo wanaoweza ni wahamiaji kutoka mataifa ya Asia, Afrika na midle east. Wazungu wengi inawashinda sana kwa sababu ya sheria zake, ila hawa wa kutoka mataifa niliyosema wanajua ujanja wa kukwepa kodi ili kuziba gharama za uendeshaji, na hawaishi maisha ya kifahari ambayo yanawapa uwezo kulilinda wanachochuma kutoka biashara hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…