Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,606
- 6,672
Matumizi ya Barakoa kwa wananchi wote kwenye sehemu zenye mikusanyiko (Mass Masking) ni hatua muhimu ya kukata mnyororo wa maambukizi katika jamii.
Aidha, matokeo ni makubwa sana pale ambapo uvaaji barakoa unaenda sambamba na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni na au kutumia vitakasa mikono.
Pamoja na jitihada za kudhibiti misongamo kufanyika ni vyema pia wananchi waendelee kuhamasishwa kuvaa barakoa wanapotoka majumbani kwao pamoja na wale wote wenye dalili.
Ni muhimu kwa mtu yoyote ambaye hataweza kuwa mbali na mtu mwingine kwa zaidi ya mita moja, ahakikishe anavaa barakoa muda wote anapokuwa na mtu ambaye hakai naye nyumba moja. Uvaaji wa barakoa utasaidia kupunguza maambukizi mengine ya mfumo wa hewa;
Hivyo tunapendekeza kuwa; -

- Serikali kupitia Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Kata, Vijiji na Mitaa, ihakikishe wananchi wanaelimishwa namna sahihi ya kuvaa, kuvua, kufua, kupasi na kutunza barakoa.
- Mamlaka za Wilaya/Halmashauri Kata na Serikali za Mitaa zihakikishe zinaelimisha na kufanya ufuatiliaji zaidi wa uvaaji wa barakoa za aina zote katika maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko
- Kwenye daladala, mabasi na magari mengine ya abiria, lazima kila dereva na kila abiria avae barakoa;
- Kwenye maeneo yote ya mikusanyiko kama sokoni, dukani, stendi, saluni, hospitali, viwanja vya ndege, kwenye meli/mtumbwi, gengeni, kanisani, mashuleni/vyuoni, mabaa, harusi, sherehe au mikutanoni, kila mmoja avae barakoa.
- Elimu itolewe ya kutosha kuhusiana na utengenezaji, matumizi sahihi na utupatikanaji wa Barakoa.
- Elimu juu uandaaji, uuzaji, Uvaaji na utumiaji sahihi wa Barakoa utolewe kwa umma kuanzia ngazi ya Kaya na Mitaa.